DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE

DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE
kiungo : DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE

soma pia


DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE

*Ataka kila muhimili uachwe ufanye kazi kwa mujibu wa Katiba 
*Agusia pia uhaba wa Majaji, azindua Mahakama inayotembea 

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

RAIS Dk. John Magufuli ameeleza kuwa katika uongozi wake amejitahidi kuhakikisha haingilia muhimili mwingine huku akisisitiza kuwa kuna ushirikiano mzuri kati ya muhimili mmoja na mwingine katika kutekeleza majukumu yao.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambapo pamoja na mambo mengine amesema Serikali,Bunge na Mahakama kila mmoja kwa nafasi yake umekuwa ukitekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba ya nchi na kwamba hata akiona baadhi ya watu wanatukana anachokifanya ni kubadilisha chaneli.

Rais amefafanua ni vema watumishi au watendaji wa mihimili hiyo wakahakikisha wanaendeelea kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi ya nchi yetu.Rais ambaye mbali ya kutoa maelezo hayo amezindua Mahakama inayotembea.Kuhusu kila muhimili kufanya kazi yake kwa mujibu wa Katiba, Rais Magufuli amesema hata yeye amekuwa makini kwa kuhakikisha anajitahidi kufanya kazi zake bila kuingilia muhimili mwingine na tangu ashike nafasi hiyo amekuwa makini katika hilo na kwamba amesisitiza kila mmoja wetu kufanya kazi kwa kufuata taratibu na 
sheria.
"Tangu niwe kwenye nafasi hii nimekuwa nikijitahidi kufanya kazi kwa kufuata utaratibu na sheria na ndio maana hajawahi kuingilia muhimili wowote.Leo hii nimefurahi kumuona Spika wa Bunge yupo hapa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo, Waziri Mkuu na viongozi wengine, hii inathibitisha namna ambavyo mihimili yetu ambavyo inafanya kazi kwa ushirikiano,"amesema.

Kuhusu Siku ya Sheria ,Rais Magufuli amesema ametumia nafasi hiyo kumpongeza Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Musa kwa uongozi wake na katika kipindi kifupi cha uwepo wake kwenye eneo la Mahakama kuna mabadiliko makubwa.Pia amesema anatambua changamoto zinazowakabili watumishi wa Mahakama na idara nyingine lakini amewaomba zisiwakatishe tamaa kwani hata zikimalizike zote zitajitokeza zingine tu.

Hivyo amewaomba waendelee kufanya kazo kwa bidii na kwamba atachambua changamoto hizo na zile ambazo zinaweza kutafutiwa ufumbuzi wake haraka atafanya hivyo."Nieleze tu ukweli karibu taasisi zote zinachangamoto ikiwemo ya uhaba wa watumishi na pamoja na Serikali kuajiri watumishi 52,000 ambao wamegawanyika katika sekta mbalimbali lakini bado uhaba upo.Ni vema kila idara ikatumia watu walionao kwa uaminifu mkubwa kwa lengo la kukabiliana na changamoto zilizopo ambapo kiukweli haziwezi kumalizika kwa wakati mmoja,"amesema.

Akizungumzia baadhi ya maombi ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma ambaye amezungumzia uhaba wa majaji, Rais Magufuli amesema licha ya uteuzi wa majaji ambao ameufanya hivi karibuni bado kuna haja ya kuwatumia Mahakimu ambao wanasifa ujaji ili kukabiliana na msongamano wa kesi."Natambua kwa mujibu wa kifungu... cha Sheria kuna Mahakimu ambao waliteuliwa 
na Waziri husika, nadhani wale wanaweza kufanya kazi za ujaji ,najua wapo kama 
195 hivi watumike ili kukabiliana na uhaba huu," amesisitiza Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Magufuli ameitaka Mahakama kusimamia haki za wamama wajane kwani wamekuwa wakipata changamoto nyingi katika kupata haki zao hasa katika suala linalohusu mirathi.
"Jaji Mkuu na hapa niseme kama kuna uwezekano wa kupata gari lingine la Mahakama inayotembea basi ni vema ikatembea huko kwa wananchi kwa maana wajane hawa wanapata tani sana.Pia nimuombe Mwakilishi wa Benki ya Dunia kuangalia uwezekano wa kupata gari nyingine hata kama mawili ili kusaidia kundi hilo kubwa la akina mama wajane,"amesema.

Kwa upande wake Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema ili Muhimili wa Mahakama uendelee kufanya kazi zake vizuri unahitaji ushirikiano kutoka kwa wananchi huku aliwataka wananchi kusoma Sheria na si lazima hadi wasome shuleni.

"Rais hapa nawaomba pia wananchi wajaribu kusoma Sheria kupitia vitabu mbalimbali ili angalau kupata uelewa wa mambo yanayohusu Sheria na kuepuka kuelekezwa katika kila kifungu cha Sheria na hata Mpiga chapa wa Serikali anatakiwa aweke sheria zote mtandaoni kwa lengo la kumrahisishia mwanachi kusoma Sheria,"amesema Prof.Juma.Amemueleza Rais Magufuli mafanikio mbalimbali na hatua ambazo wamezichukuwa hususani kwa watumishi ambao walipatikana na makosa ya rushwa na hata vyeti isivyokuwa na sifa .

Kuhusu Mahakama ya kutembea Prof.Juma amemueleza Rais Dk.Magufuli kuwa Mahakama hiyo itaaza kutoa huduma katika mikoa miwili, mkoa wa Dar es Salaam katika maeneo ya Bunje B iliyopo wilayani Kinondoni, Buza wilayani Temeke, Chanika wilayani Ilala, na katika mkoa wa Mwanza maeneo ya Busweru,Buhongwa,pamoja na Igoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe. Job Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma wakati alipowasili kuhudhuria  maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Februari 6, 2019.



Hivyo makala DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE

yaani makala yote DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/dkmagufuli-asema-katika-uongozi-wake.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DK.MAGUFULI ASEMA KATIKA UONGOZI WAKE ANAJITAJIDI KUTOINGILIA MUHIMILI MWINGINE"

Post a Comment