title : GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA
kiungo : GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA
GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Profesa Florens Luoga amesema kuwa kupeana taarifa za mikopo kunapunguza tofauti ya upatikanaji wa taarifa miongoni mwa wakopeshaji na wakopaji na kupunguza gharama za kutafuta taarifa hizo na hivyo kuboresha upatikanaji wa mikopo kwa sehemu kubwa ya wananchi.
Prof.Luoga ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kuelimisha umma kuhusu taarifa za mikipo na elimu ya fedha.Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alipaswa kuwa Waziri wa Fedha lakini kutokana na majukumu mengine amewakilishwa na Gavana wa BoT.
Akifafanua zaidi wakati wa uzinduzi huo , Profesa Luoga amefafanua kampeni hiyo ya uhamasishaji na elimu kwa umma kuhusu taarifa za wakopaji ambayo imeandaliwa na BoT kwa kushirikiana na International Finance Corporation, ambalo ni mwanachama wa Kundi la Benki ya Dunia.
"Elimu kuhusu masuala ya fedha ni muhimu katika mfumo mzima wa taarifa za mikopo. Kampeni hii ya elimu kwa umma inalenga kuwaelimisha watumiaji wa huduma za fedha na wadau wengine kukuza uelewa wao kuhusu taarifa za mikopo ili kuongeza ushiriki katika matumizi ya taarifa za mikopo hapa nchini.
"Mpango huu ni sehemu ya mpango mpana zaidi wa kukuza elimu kuhusu masuala ya fedha kwa lengo la kukuza huduma jumuishi za kifedha Tanzania kutoka asilimia 65 mwaka 2018 hadi asilimia 75 ya watu wazima wanaotumia huduma za kifedha ifikapo mwaka 2022,"amesema.
Ameongeza kampeni hiyo inaangalia masuala muhimu kuhusu taarifa za mikopo ambazo ni pamoja na maana ya taarifa ya mikopo, kwa nini taarifa hizo ni muhimu kwa wakopaji na wakopeshaji, namna gani watumiaji wa huduma za fedha wanaweza kupata taarifa za mikopo, umuhimu wa kuwa na historia nzuri ya ukopaji na umuhimu wa kuangalia taarifa zako za mikopo mara kwa mara kutoka taasisi zinazoandaa taarifa hizo ili kuhakikisha taarifa za mikopo zinakuwa nzuri.
Prof. Luoga amesema BoT ilizindua mfumo wa taarifa za mikopo Septemba mwaka 2012 ilipotoa kanuni zilizotokana na Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka
2006, yaani kanuni za Kanzidata ya Taarifa za Mikopo za mwaka, 2012 na Kanuni za Kampuni za Taarifa za Mikopo, 2012. "Hivi sasa kuna taasisi mbili zinazoandaa taarifa za mikopo ambazo zimesajiliwa na zinazofanya kazi hapa Tanzania. Taasisi hizo ni Dun & Bradstreet Credit Bureau
Tanzania Limited na Creditinfo Tanzania Limited,"amesema.
Amesema taasisi hizo zinapata taarifa zake kutoka Kanzidata ambayo inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania na taarifa (data) nyingine kutoka taasisi zingine zinazotoa huduma mbalimbali, kama kampuni za simu, wakala wa kukusanya madeni, wauzaji wa jumla na reja reja wanaotoa bidhaa na huduma kwa mkopo, taasisi za umma kama vile Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na Masijala za Mahakama.
Amesema taasisi zinazoandaa taarifa za mikopo hutayarisha taarifa hizo na kuzitoa kwa wakopeshaji na watumiaji wengine kwa ada fulani wanapozihitaji ili kuweza kujua hali ya kifedha ya watu wanaotaka kupata mikopo kutoka kwao na kwamba taarifa za mikopo ni muhimu pia kwa watumiaji wengine, ikiwemo BoT kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya fedha, wakala za serikali na sekta nyingine katika uchumi kama waajiri, watoa huduma za bima, wauzaji wa jumla na reja reja, kampuni za karadha na mawakala wa mikopo ya nyumba.
"Aidha, kushirikishana taarifa za mikopo kunachangia katika kujenga nidhamu ya ukopaji kwa kuepuka kukopa bila sababu na kuchukua mikopo mikubwa. Kwa wakopeshaji, taarifa za mikopo zinarahisisha kuangalia vihatarishi na kufanya maamuzi bora wakati wa kutoa mikopo kwa taasisi na wajasiriamali wadogo pamoja na kufuatilia wakopaji kwa ufanisi zaidi,"amesema.
Prof.Luoga amesema pia kubadirishana taarifa sahihi kati ya taasisi za fedha na wadau wote ni muhimu katika mchakato wa maamuzi, kupunguza gharama ya mikopo na wakopaji wasiolipa madeni yao. Katika kipindi cha muda mrefu, mfumo huu unatarajiwa kuchangia kupunguza gharama za mikopo, mikopo chechefu na kukuza uthabiti wa sekta ya fedha.
Amefafanua faida za kuwaruhusu wakopaji kupata taarifa zao za mikopo ni kujenga uaminifu, uwazi na usahihi wa taarifa. Ili kuhakikisha kwamba matakwa ya kisheria na usimamizi na kukuza kukubalika kwa mfumo wa taarifa za mikopo, Benki Kuu ya Tanzania inasimamia uendeshaji wa Kanzidata ya Taarifa za Mikopo na Taasisi zinazoandaa taarifa za mikopo.
Amesea BoT imekuwa ikifanya kazi ya kukuza mfumo wa taarifa za ukopaji ili kuboresha usimamizi wa vihatarishi vya mikopo katika benki na taasisi za fedha na taasisi nyingine zinazotoa mikopo, lengo likiwa ni kuongeza upatikanaji wa mikopo na kukuza huduma jumuishi za kifedha.
Prof.Luoga amesema katika kufanya hivyo, pamoja na mambo mengine walihitaji kupata msaada wa kitaalamu kutoka Benki ya Dunia kupitia shirika lake tanzu la International Finance Corporation katika maeneo manne ambayo ni kuimarisha uwezo wa Benki Kuu ya Tanzania kudhibiti na kusimamia shughuli za taarifa za mikopo;
Pia kuwezesha kuunganishwa kwa huduma ndogo za fedha na taasisi zingine za mikopo ambazo hazisimamiwi katika mfumo wa taarifa za mikopo, kusaidia uimarishaji wa elimu kwa wadau na uhamasishaji kuhusu taarifa za mikopo na usaidia uanzishaji wa Kikosi Kazi Cha Wadau kushirikiana katika kuboresha na kuendeleza mfumo wa ubadilishanaji taarifa za mikopo.
Hivyo amesema uzinduzi huo unaonesha jitihada za BoT na wadau wengine katika kukuza uelewa kuhusu mfumo wa taarifa za mikopo na elimu ya fedha kama vitu muhimu katika uendeshaji wa soko la mikopo, uthabiti wa sekta ya fedha na maendeleo ya uchumi wa taifa kwa ujumla.
"Inatarajiwa kupitia kampeni hii ya uhamasishaji, wadau mbalimbali watajua faida za kutumia mfumo wa taarifa za mikopo. Ujumbe utaelekezwa kwa wakopeshaji na wakopaji kwa lengo la kuongeza ufahamu juu ya umuhimu wa taarifa za mikopo na faida kwa makundi yote mawili,"amesema.
Hivyo makala GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA
yaani makala yote GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/gavana-benki-kuu-azungumzia-umuhimu-wa.html
0 Response to "GAVANA BENKI KUU AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUPEANA TAARIFA ZA MIKOPO,ELIMU YA FEDHA"
Post a Comment