title : AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA
kiungo : AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA
AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA
Asasi ya kitaifa inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia, Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) imeendesha kikao kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za mradi wa DREAMS unaolenga kuwafikia mabinti wa rika balehe na wanawake wadogo katika vituo 12 vya kwenye halmashauri za wilaya za Ushetu,Msalala,Kahama Mji na Manispaa ya Shinyanga.
Kikao hicho cha siku mbili kimefanyika Februari 21 na 22,2019 katika ukumbi wa Virgimark Hotel Mjini Shinyanga kwa kukutanisha pamoja mabinti wenye umri kati ya miaka 15 – 19pamoja, wanawake wadogo wenye umri wa miaka 20 -24 na watoa huduma kwenye vituo vya afya. Afisa Miradi na Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Nastervella Rweyemamu alisema kikao hicho ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa DREAMS (Determinant, Resilient, Empowered, AIDS free, Mentored Safe) wenye lengo la kuifikia jamii na kuipatia elimu kuhusu masuala ya afya hususani afya ya uzazi,ukatili wa kijinsia na upimaji wa Virusi vya UKIMWI.
“Tunaifikia jamii lengwa kupitia waelimishaji rika hawa ambao walipewa mafunzo maalum ili watoe elimu katika ngazi ya jamii wakishirikiana na watoa huduma kwenye vituo vya afya 12 ambako tunatekeleza mradi huu”,alieleza Nastervella. Alivitaja vituo vya afya 12 ambavyo vinashiriki katika mradi huo kuwa ni Kituo cha afya Ukune,Ushetu,Chela,Lunguya,Kambarage pia zahanati ya Kagongwa,Chambo,Segese,Isaka na hospitali ya Kolandoto,Kahama na hospitali rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Nastervella aliwataka waelimishaji rika kuongeza wigo kwenye huduma zao na kuhakikisha wanawafikia mabinti na wanawake wengi zaidi katika jamii ili kuwapatia elimu hali ambayo itachangia wajitambue na kutokomeza vitendo vya kikatili vinavyochangia hatari ya kupata maambukizi ya VVU na mimba zisizotarajiwa.
Nao wajumbe wa kikao hicho walisema miongoni mwa majukumu yao ni kutoa elimu kwa mabinti kuhusu mabadiliko ya tabia,kushawishi mabinti kupata huduma za afya ikiwemo kupima VVU lakini pia huduma za afya ya uzazi. “Jukumu letu jingine ni kuhamasisha mabinti kujiunga kwenye vikundi vya DREAMS na kuwashauri mabinti na wanawake wanaofanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kubakwa,kupigwa watoe taarifa haraka iwezekanavyo ili hatua za haraka ziweze kuchukulia ikiwa ni pamoja na kupatiwa huduma za dharura za kuzuia mimba na maambukizi ya VVU”,alisema Catherine Makenzi kutoka halmashauri ya Msalala. “Tunahamasisha mabinti kujiunga kwenye vikundi ambavyo husimamiwa na vituo vya afya na kupitia vikundi hivyo elimu mbalimbali hutolewa lakini pia kuwaunganisha kwenye huduma watu waliofanyiwa vitendo vya kikatili”,aliongeza Afisa Tabibu,John Bundu kutoka kituo cha afya Ukune halmashauri ya Ushetu.
Februari 21,2019 : Afisa Miradi na Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Nastervella Rweyemamu akizungumza kwenye kikao cha Waelimishaji rika na watoa huduma kutoka kwenye vituo 12 vya afya katika halmashauri za wilaya ya Kahama Mji,Msalala,Ushetu na Manispaa ya Shinyanga ambako mradi wa DREAMS unatekelezwa. Picha zote na Kadama Malunde1 blog
Afisa Miradi na Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Nastervella Rweyemamu akielezea malengo ya kikao hicho.
Waelimishaji rika wakiwa ukumbini.
Afisa Miradi na Huduma Unganishi kwa Jamii AGPAHI mkoa wa Shinyanga,Nastervella Rweyemamu akizungumza na wajumbe wa kikao hicho.
Februari 22,2019 :Catherine Makenzi kutoka Msalala akichangia hoja wakati wa kikao hicho kuhusu namna ya kuwafikia mabinti na wanawake wadogo wengi zaidi katika jamii.
Afisa Tabibu John Bundu kutoka kituo cha afya Ukune halmashauri ya Ushetu akichangia hoja wakati wa kikao hicho.
Wajumbe wa kikao hicho wakiwa ukumbini.
Mabinti wakijadiliana namna ya kuwaelimisha mabinti na wanawake wadogo/vijana katika jamii kuhusu masuala ya afya. Kulia ni Hadija kutoka zahanati ya Kagongwa akiongoza majadiliano.
Kazi za makundi kujadili maana ya DREAMS na majukumu ya waelimishaji rika katika jamii ikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Kazi za vikundi zikiendelea.
Catherine Kulwa kutoka hospitali ya Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga akiwasilisha kazi ya kikundi chake kuhusu malengo ya mradi wa DREAMS.
Mwakilishi wa kundi la pili,Aisha Mtambo kutoka kituo cha afya Ukune halmashauri ya Ushetu akiwasilisha kazi ya kundi lake kuhusu majukumu ya waelimishaji rika katika jamii.
Wajumbe wa kikao ambao ni wanakikundi cha DREAMS hospitali ya Kahama wakiwa na bidhaa zao za ujasiriamali wakati wa kikao hicho.
Kikao kinaendelea.
Picha ya pamoja wajumbe wa kikao cha Waelimishaji rika.
Picha ya pamoja. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Hivyo makala AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA
yaani makala yote AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/02/agpahi-yakutanisha-mabinti-na-wanawake.html
0 Response to "AGPAHI YAKUTANISHA MABINTI NA WANAWAKE WADOGO KUJADILI UTEKELEZAJI WA MRADI WA DREAMS SHINYANGA"
Post a Comment