VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.

VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.
kiungo : VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.

soma pia


VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.

Na Yeremias Ngerangera,Namtumbo.

Mradi wa maji katika kijiji cha Likuyusekamaganga wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma umeingia dosari baada ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vya kutekeleza mradi huo kuteketea kwa moto na watu wasiojulikana.

Mwakilishi wa kampuni ya Elegance Developers Company Ltd ya Dar es salaam inayojenga mradi huo,  fundi Ramadhan Abrahaman alisema vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 500 vimeteketezwa kwa moto na watu wasiojulikana .

Kaimu Mtendaji wa kata ya Likuyuseka bwana Petro Nyoni alidai jeshi la polisi linawashikilia watu wawili kuhusiana na tukio hilo akiwemo mlinzi wa kambi bwana Ramadhani Salumu Liyoka pamoja na Athumani Awami Kimbengite .

Aidha bwana nyoni alisema Serikali ya kijiji inatarajia kufanya kikao cha kulijadili swala hilo pamoja na baraza la wazee wa kijiji hicho nao wanatarajia kufanya kikao cha kujadili mienendo mibaya ya kijiji hicho ,kubaini chanzo cha kuibuka kwa matukio mabaya kijijini hapo na kutafuta njia sahihi za kutatua au kudhibiti matukio mabaya yasiendelee kutokea kijijin hapo.

Mhandisi mshauri bwana Nashoni Charles kutoka kampuni ya Norplan Tanzania Ltd ya Dar es salaam alisema kitendo cha kuchoma vifaa hivyo kimeiingizia hasara kampuni lakini pia kitafanya kampuni hiyo kutumia muda mwingine kwenda kununua vifaa , huku muda wa mkataba wa utekelezaji wa mradi huo upo palepale.

Kwa mujibu wa mhandisi mshauri wa kampuni hiyo bwana Nashon alidai mradi huo wa maji wa Likuyumandela umefikia asilimia 45 katika utekelezaji wake na unategemea kuhudumia watu 13,319 kwa kipindi cha miaka kumi baada ya kukamilika kwake.

Kaimu Mhandisi wa maji wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Salumu Nachundu alidai mradi unatekelezwa chini ya progamu ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP)

Gharama za ujenzi wa mradi huo ni shilingi 4,915,864,910 ikiwa mkataba wa mradi huo unategemea kukamilika tarehe 16 marchi 2019 na kiasi cha shilingi 983,172,982 zimelipwa kwa mkandarasi kama malipo ya awali.
 Baadhi ya vifaa vilivyoteketezwa kwa moto na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana 
Baadhi ya Mabomba ya kupitishia maji yakiwa yamechomwa moto na watu wasiojulikana.


Hivyo makala VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO.

yaani makala yote VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/vifaa-vya-milioni-500-mradi-wa-maji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIFAA VYA MILIONI 500 MRADI WA MAJI VYATEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA WILAYANI NAMTUMBO."

Post a Comment