UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.

UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.
kiungo : UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.

soma pia


UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

UMOJA wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tanzania kwa upande wa Zanzibar, leo umezindua rasmi kamati ndogo ndogo nne zitakazokuwa na majukumu mbali mbali ya kufanisha kwa ufanisi kazi za umoja huo kwa mwaka 2019/2020.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi alizitaja kamati zilizozinduliwa kuwa ni pamoja na Kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha, Kamati ya Mawasiliano kwa Umma, Kamati ya Elimu,Malezi na Mafunzo pamoja na Kamati ya Mahusiano na Taasisi za Wanawake ndani na nje ya Nchi.

Alisema kuwanzishwa kwa kamati hizo ni matarajio makubwa zaidi ni kuwafikia Wanawake na Vijana pamoja na makundi mbali mbali yaliyopo katika jamii na watoto ili kushinda Uchaguzi ujao mwaka 2020.

Katika maelezo yake Makamu Mwenyekiti huyo aliwasisitiza Wajumbe wote wa Kamati hizo kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utekelezaji wa majukumu ya msingi ya UWT pamoja na CCM kwa ujumla.

“Wanawake ni Jeshi kubwa tena la ukombozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nasaha zangu kwenu ni kwamba tutumie nafasi hii kuhakikisha tunawafikia wanawake wote hasa waliopo Vijijini na Pembezoni kwa nia ya kuwaweka karibu na kufanya nao shughuli zetu za kisiasa.

Pia Wanawake wa UWT lazima tupate Sauti zetu kila mmoja kwa nafasi yake ndani ya Umoja Wetu kuyasema mambo mema yanayotekelezwa na CCM chini ya Viongozi wetu Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wanaoendelea kusimamia kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.”, alisema Makamu Mwenyekiti Thuwayba Kisasi.

Aliwataka Wanawake nchini kushirikiana katika malezi ya Watoto ili waweze kukuwa wakiwa katika malezi na maadili bora yatakayowasaidia kupambana na changamoto za mmomonyoko wa maadili.Awali akizungumza Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo , alieleza kuwa UWT imejipanga kufanya kazi zake Kisayansi zaidi kwa lengo la kufanikisha kwa wakati malengo waliyojiwekea ndani ya Umoja huo.

Aidha alifafanua kuwa Kamati hizo zilizozinduliwa zitakuwa ni chachu ya kubuni miradi mipya ya kiuchumi itakayoongeza kipato ndani ya UWT pamoja na kupatikana fursa ya mahusiano mazuri na Taasisi mbali mbali za Wanawake Duniani.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati tekelezaji WUT Taifa Ndugu Lucy Mwakembe alisema Umoja huo utaendelea kupanga mikakati mbali mbali ya kimaendeleo ili kujiinua kiuchumi.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi akizungumza na Wajumbe wa Kamati ndogo ndogo za Umoja huo mara baada ya kuzinduliwa.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo akitoa ufafanuzi wa majukumu mbali mbali ya Kamati hizo ambazo ni nne zilizozinduliwa kutokana na Matakwa ya Kanuni ya Umoja huo.
BAADHI ya Wajumbe wa Kamati ndogo ndogo za UWT Zanzibar zilizozinduliwa leo wakiwa katika Kikao cha Awali cha utambulisho wa Kamati hizo, huko Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui.
Picha ya Pamoja ya Wajumbe wote wa Kamati Nne za UWT zilizozinduliwa.





Hivyo makala UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020.

yaani makala yote UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/uwt-zbar-yazindua-kamati-nne-za-kuchapa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UWT Z'BAR YAZINDUA KAMATI NNE ZA KUCHAPA KAZI KUELEKEA 2020."

Post a Comment