SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA

SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA
kiungo : SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA

soma pia


SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro amewapongeza Wastaafu wa Jeshi hilo kwa kumaliza utumishi wa umma wakiwa hawana kashfa yoyote ambayo ingelichafua jeshi hilo na kufanya lipoteze uhalali mbele ya wananchi.

IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Kuwaaga Askari na Wastaafu wa Jeshi na Sherehe ya Kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam .“Nawapongeza kwa kumaliza salama naomba mkawe na nidhamu ya fedha mtakayolipwa kama kiinua mgongo na mtumie kiasi hicho cha pesa kwa manufaa ya familia na jamii inayowazunguka” alisema IGP Sirro

Akizungumza katika Sherehe hizo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amewataka Wastaafu wa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakuwa raia wema na kudumisha amani katika maisha yao mapya baada ya kulitumikia Taifa kwa manufaa,ameongeza kuwa Upendo waliouonesha kwa wafanyakazi wenzao wakati wakiwa kazini wakauonyehe huko wanakoenda

“Mmekua mfano wa kuigwa kipindi chote mlichokua kazini, tunaomba mkawe raia wema huko kwa kuendelea kusimamia matukio ya uhalifu katika maeneo mtakayokua mnaishi, tunaamini nyie bado askari na mnafahamu mbinu zote za kupambana na uhalifu hivyo fahamuni tunawategemea bado,” alisema Jenerali Mabeyo

Maafisa na Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi walioagwa katika sherehe hizo walilishukuru Jeshi la Polisi kwa upendo walioupata katika kipindi cha utumishi kwa umma na kuwaasa maafisa na askari walipo kazini kulitumikia jeshi kwa uaminifu mkubwa.

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro akimpa zawadi Naibu Kamishna Mstaafu wa Polisi Hussein Laizer (kulia) ,Wakati wa Sherehe za kuwapongeza na kuwaaga Wastaafu wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha mwaka mpya 2019,Sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt.Anna Makakala akiongea na Maafisa ,askari waliopo kazini na wastaafu wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani), Kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na Kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukalibisha mwaka mpya 2019,Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiongea na Maafisa, Askari waliopo kazini na Wastaafu wa Jeshi la Polisi (hawapo pichani) kushoto ni Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na Kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019, Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na Inspekta Jenerali wa Polisi ,IGP Simon Sirro wakiingia ukumbini wakati wa Sherehe za Kuwapongeza na kuwaaga Wastaafu wa Vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi na kuukaribisha Mwaka Mpya 2019, Sherehe hiyo imefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam. 


Hivyo makala SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA

yaani makala yote SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/sirro-awapongeza-wastaafu-kumaliza-bila.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SIRRO AWAPONGEZA WASTAAFU KUMALIZA BILA KASHFA"

Post a Comment