title : RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA
kiungo : RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA
RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
ASASI ya Uzalendo nchini (AWAMATA) imemtunuku cheti cha uzalendo Rais Dkt. John Magufuli kwa kufanya vizuri katika kipengele cha uzalendo kwa mwaka 2018.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa City Garden jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Asasi hiyo Chief Daudi Mrindoko ameeleza kuwa Rais Magufuli amejitoa katika kupambana na rushwa pamoja na kuanzisha miradi mikubwa yenye lengo la kuboresha uchumi na hali ya wananchi wa kawaida, hivyo mchango wake unapaswa kutambuliwa, kuthaminiwa na kuheshimiwa.
Mrindoko amesema kuwa mipango ya Asasi hiyo ipo katika kueneza elimu ya uzalendo kwa kuanzisha chuo cha Uzalendo kitakachotoa Elimu ya Uzalendo, Ujasiriamali na kuwajengea vijana uwezo wa kujitegemea na kuwa zao bora kwa taifa.
Pia Asasi hiyo imetoa picha maalumu ya miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Magufuli katika kipindi cha mwaka 2018 na kuelezwa kuwa kuwa kasi anayoenda na Mh. Rais ni kuleta neema kwa wananchi wengi.
Mwenyekiti wa AWAMATA Chief Daudi Mwidadi Mrindoko (aliyeshika picha) na katibu wa taasisi hiyo Pilly Kimario(aliyeshika cheti kushoto) wakiwa kwenye picha ya Pamoja na wadau na washiriki wa mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam .
Mwenyekiti wa AMATA Chief Daudi Mwidadi Mrindoko (aliyeketi kushoto) na katibu wa Asasi hiyo Pilly Kimario(aliyeketi kulia)wakiwa Pamoja na wakurugenzi wapya wa Asasi waliotangazwa katika mkutano mkuu wa mwaka, jijini Dar es Salaam.
Cheti cha pongezi na kutambua mchango kupitia kipengele cha uzalendo kwa mwaka 2018 kilichotolewa na taasisi ya uzalendo nchini kwa Rais Dkt.John Magufuli, jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA
yaani makala yote RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/rais-dkt-magufuli-atunukiwa-cheti-cha.html
0 Response to "RAIS DKT. MAGUFULI ATUNUKIWA CHETI CHA UZALENDO NA AWAMATA"
Post a Comment