title : RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA
kiungo : RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA
RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
RAIA wa Pakistani, Muhammad Hasnaih Hyderi leo Januari 17,2019 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutaka kumpa rushwa Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Imedaiwa na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (Takukuru), Pascal Magabe akisaidiana na wakili, Leornad Swai kuwa, Januari 15, 2019 huko katika Mgahawa wa Best Bite uliopo ndani ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitenda kosa.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza imedaiwa, siku ya tukio mshtakiwa alitoa rushwa ya Sh. milioni mbili kwa Talib Kombo ambaye ni Ofisa wa TRA) ili kumsaidia asilipe kodi kubwa.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande Kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka kuwa na wadhamini wawili kutoka ofisi yoyote inayotambulika na Serikali watakaosaini bondi ya Sh.milioni tano kila mmoja.
Pia Mahakama imemtaka mshtakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria na haruhusiwi kusafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama.Kwa mujibu upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo umeisha kamilika na kesi hiyo itatajwa Januari 31 mwaka huu
MtuhumiwaRAIA wa Pakistani, Muhammad Hasnaih Hyderi leo Januari 17.2019 akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kutaka kumpa rushwa afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hivyo makala RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA
yaani makala yote RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/raia-wa-pakistan-afikishwa-kortini-kwa.html
0 Response to "RAIA WA PAKISTAN AFIKISHWA KORTINI KWA SHTAKA LA KUTAKA KUMPA RUSHWA OFISA WA TRA"
Post a Comment