PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE

PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE
kiungo : PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE

soma pia


PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE

*Ni wakati tukio la utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya TFS na NLUPC


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAKATI mjadala ukiendelea kuhusu tukio la bundi kutumia Bungeni, leo hii katika tukio la utiwaji saini wa mkataba wa ushirikiano kati ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi(NLUPC) Paka a.k.a Nyau ameingia katika ukumbi wa mikutano wa Mpingo House jijini Dar es Salaam.

Paka huyo aliingia ukumbini hapo saa sita kasoro dakika tano ikiwa ni dakika chache kabla ya tukio la utiwaji saini kufanyika ambapo haijulikani alitokea wapi.Wakati anaingia ukimbini Paka huyo alianza kupiga kelele za milio ule maaruf wa Nyauuuu...nyau...nyau... kwa staili yao kama ambavyo tumezoea kuusikia masikioni.

Baada ya kuingia ukumbini hakuwa na makeke kwani baada kufika alikwenda kukaa pembeni ya ukutano na kisha akajituliza tuli.

Baadhi ya waandishi waliokuwa ukumbini hapo walijikuta wakianza kucheka kutokana na Paka huyo kuingia.Kwa kuwa hakuna na vurugu yoyote kilichobaki ikawa ni kumuangalia na kwa huu ni ulimwengu wa teknolojia ,kilichofuata ikawa ni kumpiga picha(kama unavyoona hapo pichani).

Hata hivyo baadhi ya waandishi waliamua kumfuata ili kumuondoa mahali alipo lakini aligoma kuondoka.Wakati Paka huyo akiwa mkutanoni hapo waliokuwa meza kuu na wale wa viti vilivyokuwabna baadae akaamua kusogea.

Hivyo wakati wa utiwaji saini mkataba huo aliondoka ukumbini na baada ya tukio kukamilika akarejea tena.

Ujio wake kwa mara ya pili ulisababisha baadhi ya waandishi kujiuliza na maswali kuhusu Paka huyo ambapo baadhi yao wakajikuta wakizungumzia tukioa Bundi kutua Bungeni ambapo Spika wa Bunge Job Ndugai aliamua kuelezea tukio hilo na kwamba kwa Dodoma Bundi wa usiku ndio mwenye madhara na si bundi anayeonekana mchana.

Haifahamiki Paka aliyeingia ukumbi wa mikutano wa Mpingo House leo alikuwa na mkakati gani.Hiyo itabaki kuwa siri ya Paka mwenyewe.



Hivyo makala PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE

yaani makala yote PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/paka-aka-nyau-aingia-ukumbi-wa-mikutano.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "PAKA A.K.A NYAU AINGIA UKUMBI WA MIKUTANO WA MPINGO HOUSE"

Post a Comment