title : Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya
kiungo : Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya
Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii
KESI ya uchochezi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama wao, Freeman Mbowe inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imepangwa kuendelea kusikilizwa kwa Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina.
Hatua hiyo imekuja baada ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi Wilbard Mashauri kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Aidha, rufaa iliyokatwa na upande wa serikali kupinga uamuzi mdogo wa Mahakama Kuu wa kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya kufutiwa dhamana kwa Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Rufani Februari 18, mwaka huu.
Mapema, wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameeleza mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo Januari 31.2019 imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba rufaa iliyopo Mahakama ya Rufani bado haijasikilizwa, hivyo aliomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata hivyo, wakili wa utetezi, Profesa Abdallah Safari ameieleza mahakama kuwa rufaa imepangwa kusikilizwa Februari 18, 2019.Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, mwaka huu na kuwaeleza washitakiwa walio nje kwa dhamana kuwa dhamana zao zinaendelea Mbowe na Matiko wamerudishwa rumande.
Novemba 23, mwaka jana Jaji Mashauri akiwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kwa sababu walikiuka masharti ya dhamana.Baada ya maamuzi hayo, washitakiwa wakiwakilishwa na Wakili wao Peter Kibatala walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga maamuzi ya mahakama hiyo ya kufuta dhamana.
Hata hivyo, baada ya mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo.Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulikata rufaa kupinga maamuzi yaliyotolewa na kuiomba mahakama hiyo kuacha kuendelea kusikiliza rufaa hiyo kwa sababu haina mamlaka.
Kufuatia hayo, Jaji Rumanyika alisema mahakama yake imefungwa mikono hivyo anasitisha usikilizwaji wa rufani hiyo hadi hapo itakapotolewa uamuzi katika Mahakama ya Rufani.
Mbali na Mbowe na Matiko washtakiwaa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu ambao wote walikuwepo mahakamani.
Katika kesi ya msingi, washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa chama wao, Freeman Mbowe akizungumza jambo na Mh.Lazaro Nyarandu.
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Chadema wakijadiliana jambo
Baada ya Hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 14,
Hivyo makala Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya
yaani makala yote Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kesi-ya-uchochezi-dhidi-ya-vigogo-wa.html
0 Response to "Kesi ya uchochezi dhidi ya vigogo wa Chadema yapata Hakimu mpya"
Post a Comment