NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI

NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI
kiungo : NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI

soma pia


NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI


NA LUSUNGU HELELA-GEITA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu amewaonya wananchi wanaofanya shughuli za kibinadamu ndani ya Hifadhi za Misitu nchini kuacha tabia ya kuwashambulia Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Onyo hili linakuja ikiwa zaidi ya watumishi watano wa TFS katika mikoa ya Pwani, Tabora ,Kigoma pamoja Kilimanjaro wakiwa wamepoteza maisha yao kwa kushambuliwa na wananchi wakati wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Aidha, Mhe.Kanyasu amepiga marufuku kwa watumishi wa TFS kujichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga wananchi wanapobainika kutenda makosa."Watumishi wa TFS hamruhusiwi kumpiga Mwananchi mnapomkamata ndani ya Hifadhi au akiwa anasafirisha mazao ya Misitu kinyume na sheria, atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Ametoa onyo hilo wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mgusu wilayani Geita mkoani Geita ikiwa ni ziara yake ya kutatua migogoro ya mipaka kwenye msitu wa Hifadhi Geita iliyopo baina ya Vijiji ambapo jumla ya hekta 4,462.95 zimefutwa kwa tangazo la Serikali.

Amesema shughuli za uhifadhi ni lazima zifanyike kwa ushirikishwaji kati ya wananchi na watumishi wa TFS." Uhasama unaozidi kujengeka kati yenu hauna tifa katika uhifadhi shirikianeni" amesisitiza Mhe.Kanyasu.Amewataka wananchi kuheshimu na kuzifuata sheria za uhifadhi ya Misitu nchini huku akiwataka watumishi kujiepusha na migongano kati yao na wananchi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Geita mkoani Geita akipewa maelezo na Meneja wa Misitu wa wilaya wa Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania (TFS) Fedy Ndandika wakati alipotembelea eneo la Manga lililokuwa limevamiwa na wakulima ambayo ni moja ya eneo la Msitu wa Hifadhi Geita
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu, Halmashauri ya wilaya ya Geita mkoani Geita akiwasisitiza wananchi umuhimu wakufuata sheria na kuacha tabia ya kuvamia Hifadhi za Misitu.
Mkazi wa kata ya Mgusu, Anaeli Mbokile akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwasilisha ombi la kumegewa eneo la Hifadhi ya Msitu Geita ili liweze kutumika kwa ajili ya malisho na makazi baada ya wakazi wa kata ya Mgusu idadi ya kuongezeka.
1. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiteta jambo na baadhi ya wanachama wa CCM wakati alipomaliza mkutano wa hadhara katika kata ya Mgusu mkoani Geita. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA).


 


Hivyo makala NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI

yaani makala yote NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-waziri-kanyasu-awafunda-watumishi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WATUMISHI WA TFS PAMOJA NA WANANCHI"

Post a Comment