title : NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA.
kiungo : NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA.
NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge kazi ,Vijana ,Ajira na wenyeulemavu Mhe. Stella Ikupa akikabidhi mguu bandia kwa mmoja wa walemavu waliopatiwa miguu hiyo katika hafla iliyo fanyika Oysterbay jijini Dar es salaa ,wamwisho kushto ni Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa, Ritha Kabati ,aliyesafirisha walemavu 25 kutoka mkoani kwake.(Picha na John Luhende)
Na .John Luhende
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge kazi ,Vijana ,Ajira na wenyeulemavu Mhe. Stella Ikupa, amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua na kufanya jitihada mbalimbali kuwatambua na kutatua changamoto zinazo wakabili watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mhe. Ikupa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, alipokuwa mgenirasmi katika hafla ya kugawa viungo bandia kwa zaidi ya watu wenye ulemavu 120 kutoka mikoa mbalimbali nchini. kuwasaidia iliyoandaliwa na Kampuni ya Kamal steal group kwa kushirikiana na taasisi ya kuwezesha jamii PEF, nakuitaka jamii kuwa na moyo wa kusaidia wengine hasa kundi lenye uhitaji maalumu.
"Naomba Jamii ielewekuwa kutoa ni moyo siku kwamba Kamal ndiyo wana fedha nyingi sana na hazina kazi, ni moyo wa utoaji nakuona kuwa hikikidogo nilichonachonigawane na wengine sote tunapaswa kuwa na moyo huo" Alisema.
Aidha ameitaka jamii kutenda mema nakusema kuwa mtu anapowasaidia wanyonge anaanza mbegu njema hatakizazichake cha nne hatakamaumetumiapesakiasigani akifa mema hayo watatendewa kikazi hicho na ameniwekea hazina kwa Mungu.
Pia amewataka watu wenye ulemavu kuto mlaumu Mungu kwa hali waliyonayo bali watumie viungo alivyo navyo kwaajili ya kujiletea Maendeleo.
"Jambo la kwanza unapaswa kumshukuru Mungu kwa kile ambacho kimetoka kwenye maisha yetu na baada ya kupata hivi viungo tuangaliefursa zainazotuzunguka ili tuweze kujiletea Maendeleo na Taifa kwa ujumla" Alisema.
Mwenyekiti wa Kamal Group, Gagan Gupta amesema kampuni hiyo imetoa zawadi ya mwaka mpya kwa watu wenye ulemavu ili waweze kufanya kazi za kujipatia riziki na kurejesha furaha yao.
Gupta amesema msaada huo unatolewa kupitia mfuko wake wa Uwezeshaji wa Wananchi (Peoples’ Empowerment Foundation - PEF), Kamal Group kwa kushirikiana na Klabu ya Rotari ya Bahari Dar es Salaam imetoa miguu bandia yenye thamani ya mamilioni ya fedha kwa watu 120.
"Hii ni mara ya nne kwa kampuni ya Kamal kutoa zawadi kwa walemavu na mpaka sasa tumewafikia 370 na waliopata wanaendelea na kazi zao kama kawaida," Amesema.
Baadhi ya watu wenye ulemavu wamesema zawadi watakayopata inazidi thamani ya pesa kwa sababu baadhi yao walikata tamaa kimaisha kwa kukosa viungo.
"Nashukuru kupata mguu naamini nitaweza kumaliza masomo yangu ya sekobdari kwa amani," amesema Omary Iddy mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Highland ya mkoani Iringa.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa, Ritha Kabati aliyesafirisha walemavu 25 kutoka katika mkoa wake wamesema viungo wanavyopatiwa walemavu hao vitawafanya wengi watimize ndoto zao kimaisha.
" Viungo hivi vitapunguza utegemezi kwa sababu hawa watakaopewa wataweza kufanya kazi na kuinuka upya, kampuni hii imefanya kazi nzuri natamani kuona nyingine zinaiga mfano katika kutatua matatizo ya jamii," amesema.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA.
yaani makala yote NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-waziri-ikupa-atoa-somo-kwa.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI IKUPA ,ATOA SOMO KWA WALEMAVU AKIGAWA MIGUU BANDIA."
Post a Comment