TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE

TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE
kiungo : TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE

soma pia


TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE

 Image result for PICHA ZA TUNDU LISSU

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amedai kuwa kuna mkakati wa kutaka kumvua Ubunge kwa madai kuwa ni mtoro bungeni.

Akizungumzia kwa undani mkakati wa kutaka kumvua Ubunge, kupitia waraka wake alioutoa, Lissu alidai kuwa kuna hoja inajengwa kuwa Mbunge huyo ni mtoro kwani hajaonekana Bungeni na hajamwandikia barua Katibu wa Bunge taarifa yoyote ya maandishi kuhusu kuumwa kwake wala matibabu yake.
 
Mbunge huyo ameeleza kuwa  hana sababu yoyote ya kutilia shaka taarifa hizi kwani waliomtonya ni watu wenye dhamana kubwa Bungeni na Serikalini ambao alidai hawaridhishwi na mkakati huo.

“Sijashangazwa na kuwepo kwa mkakati huu.Kilichonishangaza ni hoja zinazojengwa kuhalalisha uovu huu.


“Ni taarifa gani ya maandishi watu hawa wanahitaji wakati nilishambuliwa nikiwa kwenye vikao vya Bunge Dodoma?,” alihoji Lissu na kuongeza kuwa.


“Nilipelekwa Nairobi nikiwa sijitambui kutokea Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma, baada ya kikao kilichomshirikisha Katibu wa Bunge wakati huo, Dk. Thomas Kashilila, Spika Ndugai na Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.


“Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake Dk. Ulisubisya Mpoki walikuwepo kwenye kikao hicho. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wakati huo, Mwigulu Nchemba, alikuwepo; na nilisindikizwa mpaka Nairobi Hospitali na daktari kutoka Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma, sasa taarifa gani inatafutwa,?” alihoji Lissu.


Kwa mujibu wa Lissu, wakati wote ambao amekuwa kwenye matibabu, uongozi wa Bunge umewasiliana kwa maandishi na mwakilishi wa familia yake kuhusu matibabu yake na wametoa matamko mengi hadharani kuhusu kushambuliwa kwake.


“Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amekuja kuniona nikiwa hospitalini Nairobi; Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Joseph Sokoine, amekuja kuniona hospitalini Leuven mara mbili.


“Ni Spika Ndugai na uongozi wote wa Bunge, akiwemo Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai, na maofisa wake, ndio hawajawahi kukanyaga hospitalini kuja kumwangalia mgonjwa wao, aliyeumizwa vibaya akiwa Bungeni,” amesema Mbunge huyo.


Alipoulizwa  kuhusu madai hayo, Spika Ndugai amesema hajui kama kuna mkakati wa kumvua Ubunge, lakini kwenye hoja ya utoro kweli Lissu ni mtoro.

“Kila mtu anajua Tundu Lissu ni mgonjwa na anapata matibabu Ubelgiji, sasa ukisikia ametoka Ubelgiji na kwenda sijui Uingereza na Spika hana taarifa na analipwa mshahara, huyo mtu ni mtoro, mwambieni arudi nyumbani kama ameshapona,” alisema Ndugai 

 
Ndugai alisema Lissu anapaswa kutambua kuwa hana ruhusa ya kuzurura nje ya nchi.

“Yeye ametoka kuugua aache uzushi arudi nyumbani. Kitu muhimu ni kwamba ajue hana ruhusa ya Spika ya kuwa huko anakozurura.

"Wakati wenzake tuko bungeni tunafanya kazi za wananchi yeye yuko huko nje  kuipaka matope nchi yetu.” Alisema Ndugai.
Chanzo Mpekuzi blog


Hivyo makala TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE

yaani makala yote TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/tundu-lisu-afunguka-kuhusu-ubunge-wake.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TUNDU LISU AFUNGUKA KUHUSU UBUNGE WAKE"

Post a Comment