title : HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR
kiungo : HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR
HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR
Hatimaye tamasha la Pasaka ambalo limekuwa likisindikizwa na kishindo cha muziki wa injili chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions Ltd ya jijini Dar es Salaam, limerejea tena kwa maandalizi makubwa.
Tamasha hilo kongwe ambalo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2000, kwa miaka miwili halikuweza kufanyika katika jiji la Dar es Salaam kutokana na sababu maalumu zilizowahi kuelezwa na waratibu wa tukio hilo la kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari jana Januari 21, 2019, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alisema baada ya tafakuri ya kina pia kwa kuzingatia maoni ya wadau wa muziki wa injili, wameamua kurejesha tukio hilo jijini humo.
“Kama mnavyojua, kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litatafanyika pia katika jiji hilo kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno,” alisema Msama."Kutokana na maombi ya Wadau kuw mengi kuhusu tamasha hilo, Wadau kilio chao kimesikika,hivyo tamasha hili litaanzia hapa hapa jijini Dar na kuendelea mikoa mingine ambayo itatajwa hapo baadae"aliongeza Msama
Alisema mbali ya malengo ya msingi ya kueneza ujumbe wa Neno la Mangu na sehemu ya mapato kusaidia makundi maalumu, safari hii tamasha hilo litatumika pia kuhimiza hali ya amani chini ya kaulimbiu isemayo ‘Upendo, haki na Amani ndio msingi wa amani.’
Msama alisema, kwa kuzingatia uhalisia huo tamasha hilo litabeba agenda ya kuombea amani taifa na kumwombea Rais John Magufuli aweze kuongoza kwa ufanisi na mafanikio zaidi kwa maslahi ya watanzania wote.
Kwa upande wa maandalizi, Msama alisema tofauti na miaka mingi, safari hii wamejiandaa kuhakikisha linakuwa la kimataifa zaidi ikiwemo kuwaleta waimbaji mahiri wa kutoka nje watakaoshirikiana na wengine wa Tanzania.
Mbali ya Dar es Salaam, Msama alisema tamasha hilo litafanyika pia katika mikoa mingine 10 ambayo itajulikana baadaye kwa kuzingatia vigezo stahiki vilivyowekwa na kamati ya maandalizi.
Chini ya maudhui ya msingi ya Tamasha hilo, ni kueneza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia waimbaji, kukuza muziki wa injili ili kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji vya kuimba na kumiliki jukwaa na wauzaji wa kazi za kimuziki.
Tangu kuanza kwa tamasha hilo, waratibu wamekuwa walitumia sehemu ya mapato ya viingilio kuyafariji makundi maalumu katika jamii; walemavu, yatima pamoja na wajane.
Tukio hilo ndilo limechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa injili nchini kutokana na waratuibu kuwaleta waimbaji mbalimbali wa kimataifa kama Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope wa Afrika Kusini.

Wasanii wengi wamekuwa wakishiriki katika tamasha hilo wakiwepo wa Tanzania kama Upendo Nkone, Christopher Mahangila, Rose Mhando, Sifael Mwakabuka , Matha Mwaipaja, Beatrice Mwaipaja, Joshua Mlelwa pamoja na kwaya mbalimbali, huku katika mataifa kama ya Kenya wasanii wa Injili kama Solomon Mukubwa,Kutoka Afrika kusini kama vile Solly Mahlangu, Sipho Makabane na Rabeca Malope na wengine wengi.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akizungumza jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa habari jana Januari 21, 2019,kuhusu ujio upya na maandalizi ya tamasha la Pasaka 2019,linatarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar.Msama amesema kuwa kwa miaka kama mitatu hivi, tamasha la Pasaka lilikuwa likifanyika mikoani tu, lakini kwa mwaka huu litaanzia jijini Dar kwa sababu vilio vya wadau wa muziki wa injili ni vikubwa mno
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama alipokuwa akifafanua zaidi kuhusu ujio mpya na maandalizi makubwa ya tamasha la Pasaka 2019,ambalo linatarajiwa kuanza kufanyika jijini Dar.

Hivyo makala HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR
yaani makala yote HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/hatimaye-tamasha-la-pasaka-kurejea-kwa.html
0 Response to "HATIMAYE TAMASHA LA PASAKA KUREJEA KWA KISHINDO,KUANZIA JIJINI DAR"
Post a Comment