title : NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI
kiungo : NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI
NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI
Daktari Bingwa wa wagonjwa wa moyo waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) Vivian Mlawi akimweleza Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera maendeleo ya afya ya mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na kuzibwa matundu ya moyo katika kambi maalum ya matibabu inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo kwa watoto wa JKCI, Israel na Ujerumani.
Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiangalia uzibuaji wa mishipa ya moyo iliyoziba jinsi unavyofayika katika kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Uuuguzi Robert Mallya akimweleza Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera kuhusu mendeleo ya ukarabati wa wodi ya watoto wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Katikati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel Simon Fisher na kulia ni Afisa Mipango wa JKCI Vida Mushi.
Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na wafanyakazi wa JKCI , Israel na Ujerumani mara baada ya kumalizika kwa ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu ya moyo wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua.
Balozi Naibu Balozi wa Ujerumani Nchini, Jörg Herrera akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Taasisi hiyo ili kuona maendeleo ya kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanywa kwa pamoja na madaktari bingwa wa Moyo wa JKCI, Israel na Ujerumani. Jumla ya watoto 20 wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua katika kambi hiyo ya siku tano.
Picha na JKCI
Hivyo makala NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI
yaani makala yote NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/naibu-balozi-wa-ujerumani-nchini.html
0 Response to "NAIBU BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ATEMBELEA JKCI"
Post a Comment