Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura

Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura
kiungo : Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura

soma pia


Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura

 Na Karama Kenyunko globu ya Jamii 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uchochezi inayomkabili, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa sababu shahidi aliyetakiwa kuanzakutoa ushahidi wake Leo amepata dharura.

Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi lakini Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine Kwani shahidi amepata dharura.

Mheshimiwa,  kesi Leo ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa  lakini kwa bahati mbaya amepata matatizo ya Kifamilia, hivyo wanaomba ahirisho fupi". Ameeleza Katuha

Kufuatia taarifa hiyo, wakili wa Zitto, , Jebrah Kambole amedai kuwa, mtuhumiwa leo Januari 29.2019 alijipanga kusikiliza kesi hiyo licha ya kuwa anakabiliwa na majukumu mengine. Hivyo,  ameiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi February 27, 
 Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi February 27,2019.

Zitto alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Novemba 2, 2018 kujibu mashtaka matatu ya uchochezi katika kesi ya jinai namba 327/2018.

Katika kesi ya msingi,  Zitto anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28,2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa kuwa siku hiyo akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kwa nia ya kuleta chuki miongoni mwa wananchi wa Tanzania dhidi ya Jeshi la Polisi alitoa maneno ya uchochezi.

Alitoa maneno ya uchochezi kuwa "watu ambao walikuwa ni majeruhi katika tukio la mapambano baina ya wananchi na polisi, wakiwa wamekwenda hospitali kupata matibabu katika kituo cha afya cha Nguruka, polisi wakapata taarifa kuwa kuna watu wanne wamekwenda hospitali kituo cha afya Nguruka kupata matibabu wakawafuata kule wakawaua"
Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa ni maneno ambayo ni ya uchochezi yenye kuleta hisia za hofu na chuki.


Hivyo makala Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura

yaani makala yote Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kesi-ya-zitto-yapigwa-kalenda-baada-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Kesi ya Zitto yapigwa kalenda baada ya shahidi kupata dharura"

Post a Comment