DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI
kiungo : DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI

soma pia


DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Mhe. Rwegasira Mukasa Oscar (kushoto) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi katika kikao na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliongoza ujumbe wa Wizara katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Bunge Dodoma tarehe 11 Januari 2019. Wengine katika picha, kuli ni Bw. Hamid Mbegu, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani, Bw. Japahary Kachenje. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliwasilisha taarifa mbili katika kikao hicho. Taarifa ya kwanza ilihusu hatua zinazochukuliwa na Wizara katika mapambano dhidi ya Ukimwi na taarifa ya pili ilihusu namna Wizara inavyoshirikiana na mashirika ya kimataifa, kikanda na nchi mbalimbali katika kukabiliana na biashara haramu ya dawa za kulevya. 
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ukisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zinawasilishwa na Mhe. Naibu Waziri. 
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi walioshiriki kikao hicho. 
Mhe. Amina Mollel, Mbunge wa Viti Maalum akichangia jambo wakati wa kikoa kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Mhe. Masoud Abdallah akichangia jambo katika kikao hicho. 
Ujumbe wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ulioshiriki kikao kati ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje. 
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Wizara ulioshiriki kikao hicho. 
Waheshimiwa Wabjumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi wakisalimiana na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kikao kuanza. 
Mhe. Allan Kiula, Mbunge wa Iramba Mashariki akisalimiana na Mhe. Naibu Waziri. 
Mheshimiwa Mbunge akibadilishana mawazo na Mhe. Naibu Waziri kabla ya kuanza kikao. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Joyce Kimey akiongea machache na Mhe. Naibu Waziri kabla hawajaingia katika kikao na Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi. 


Hivyo makala DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI

yaani makala yote DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dkt-ndumbaro-akutana-na-kamati-ya-bunge_12.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT. NDUMBARO AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI"

Post a Comment