DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE

DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE
kiungo : DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE

soma pia


DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani Jokate Mwegelo ameanza ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo wilayani humo kwa lengo la kuhakikisha wanatambuliwa na kufanya shughuli zao za kiuchumi bila kusumbuliwa.

Jokate ametoa vitambulisho hivyo leo kwa baadhi ya wajasiriamali wa Wilaya ya Kisarawe ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Rais Dk.John Magufuli alipozindua utoaji wa vitambulisho hivyo kwa kuwapa wakuu wa mikoa yote nchini ili vigawiwe kwa wajasiriamali.

Akizungumza leo wilayani hapo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya ambao wameshiriki kushuhudia tukio la ugawaji wa vitambulisho hivyo, Jokate amesema katika wilaya hiyo kuna wajasiriamali 502 na hivyo ugawaji huo utaendelea kwa kuhakikisha wote wanaostahili kuvipata wanapewa.

Amesema wilaya ya Kisarawe inatambua mchango wa wajasiriamali hao na kwamba wamedhamiri wote wapewe vitambulisho hivyo ambavyo pamoja na mambo mengine kwa wale ambao watakuwa na vitambulisho hivyo watafanyakazi zao za ujasiriamali bila kusumbuliwa.

"Mkuu wa Mkoa wetu wa Pwani ametukabidhi hivi vitambulisho kwa ajili ya kuwapatia wajasiriamali, hivyo leo tumeanza kuvigawa.Ni mchakato endelevu ambao tutaufanya kwa wakati na hapa kwetu tunao wajasiriamali 502, na wote tutawapa," amesisitiza Jokate.

Wakati huo huo amezungumzia mikakati ya Wilaya ya Kisarawe katika kuhakikisha wanapiga hatua ya kimaendeleo ikiwa pamoja na kuitangaza Wilaya hiyo ambayo ina fursa za kila aina za kiuwekezaji .

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akimkabidhi kitambulisho cha ujasiriamali mjasiriamali Indiana Mohamed Mnyukwa katika kikao cha RCC kinachofanyika mjini Kisarawe leo wilaya ya Kisarawe imeanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyetoa vitambulisho kwa ajili ya wajasiriamali nchini kote.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajasiriamali waliokabidhiwa vitambulisho vyao leo.


Hivyo makala DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE

yaani makala yote DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dc-jokate-mwegelo-aanza-kukabidhi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC JOKATE MWEGELO AANZA KUKABIDHI VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI WADOGO WILAYANI KISARAWE"

Post a Comment