title : Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba
kiungo : Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba
Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba
Wazanzibar wana kila sababu ya kujivunia Maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Sekta ya Elimu yaliyosimamiwa na Chama cha Afro Shirazy Party na Baadae CCM katika kipindi chote cha Miaka 55 tokea kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yaliyoondoa Utawala wa Kibaguzi katika Elimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Uweleni iliyopo Mkoani Kisiwani Pemba katika Smra shamra za kusherehekea Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 kutimia Miaka 55.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hatua iliyofikia Taifa hivi sasa katika Sekta ya Kielimu ni kubwa kiasi kwamba wale wanaokebehi wanashindwa kujifahamu kwamba wanajidharau wao wenyewe na dawa yao ni kupuuzwa kwa sababu hawajui thamani ya kuwa na chao na wala sio watu wanaothamini cha wenzao. Alisema tokea Wananchi wa Zanzibar walipojitawala kutoka katika makucha ya kibeberu, Vijana wa Visiwa hivi wanaendelea kupata Elimu bila ya malipo, kuanzia maandalizi hadi Sekondari ya Juu ambapo pia wakifikia Vyuo Vikuu kuna utaratibu wa kuwapatia udhamini kwa wale wanaofanya vizuri.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Mkoa wa Kusini Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akizungumza na Wananchi wa Pemba baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari ya Uweleni Pemba. Picha na – OMPR – ZNZ.
Haiba ya Jengo Jipya linalojengwa katika Skuli ya Sekondari ya Uweleni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba
yaani makala yote Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/balozi-seif-aweka-jiwe-la-msingi-la.html
0 Response to "Balozi Seif aweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la shule ya Sekondari ya Uweleni kisiwani Pemba"
Post a Comment