title : WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM
kiungo : WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM
WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amezindua Baraza la Famasi na kuwataka kusimamia sheria ili kudhibiti uuzwaji wa dawa katika maduka ya dawa yasiyo na vibali.
Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa, jukumu la Baraza la Famasi ni kuleta msukumo wa utoaji huduma bora ya afya kwa mtanzania. Hili linawezekana kwa kuhakikisha kuwa wanataaluma wanazingatia maadili na nidhamu ya taaluma katika ununuaji, utunzaji na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba vilivyo salama na ubora wa hali ya juu.
Amesema, anapenda nisisitize kuwa Baraza lione umuhimu wa kuweka msukumo wa pekee kwenye masuala ya kuboresha mafunzo na elimu ili tuwe na wanataaluma wenye uwezo wa utendaji wa kiwango cha hali ya juu katika nchi yetu katika maeneo yote ikiwamo uzalishaji wa dawa Viwandani ili kwenda sambamba na adhima ya Serikali kuelekea uchumi wa Viwanda.
Ummy anesema anapenda kuwahakikishia kuwa, jamii ya watanzania wanahitaji huduma hii, hali inaonesha kuwa, kupitia takwimu mbalimbali zaidi ya 40% ya wananchi wanapopata tatizo la afya huanza kwenda kupata huduma ya awali kwenye maduka ya dawa (famasi na maduka ya dawa muhimu), hivyo basi kushindwa kuwa na huduma bora katika maeneo hayo na inahatarisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wananchi.
"Wataalam wa fani ya famasia ndio wahusika wakuu katika masuala yote yanayohusu dawa katika kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini. Serikali kwa upande wake imeongeza bajeti ya Dawa kutoka Shilingi bilioni 30 mwaka 2015/2016 hadi Tsh 270 Bilioni mwaka 2018/2019, hivyo ni Wataalamu hawa wa Famasi wanaotakiwa kuhakikisha kuwa ongezeko la bajeti linaenda sambamba na upatikanaji wa dawa na matumizi sahihi kwa kuzingatia miongozo ya tiba," Ummy
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la Famasi na kuwataka kusimamia sheria ili kudhibiti uuzwaji wa dawa katika maduka ya dawa yasiyo na vibali leo Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Famasi Elizabeth Shekalaghe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Baraza la Famasi leo Jijini Dar es Salaam.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa tuzo kwa kwa wajumbe wa baraza la famasi lililomaliza mda wake, Kushoto ni Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi.
Hivyo makala WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/waziri-ummy-mwalimu-azindua-baraza-la.html
0 Response to "WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BARAZA LA FAMASI LEO JJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment