Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?

Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?
kiungo : Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?

soma pia


Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?

Sehemu mbalimbali duniani mtazamo kuhusiana na matumizi ya mmea wa cannabis yaani bangi unabadilika kwa kasi.

Serikali mpya ya Mexico ina mpango wa kuhalalisha matumizi ya bangi kama njia ya kujiburudisha, sawa na ilivyofanya utawala mpya wa Luxembourg. Wakati huo huo, viongozi wakuu nchini New Zealand, wanakusudia kuandaa kura ya maoni ya namna watakavyoshughulikia swala hilo.

Jinsi maoni ya umma - na yale ya serikali- yanavyobadilika, ni dhahiri kuwa mataifa mengi yatafuata mkondo huo. Maswali yanayoibuka ni kwa namna gani nchi hizo zitadhibiti matumizi na usambazaji wa mmea huo?

Ni nini hasa kinachopelekea mataifa mbalimbali katika kulegeza kamba kwenye sheria zake, au hata kuamua kuidhinisha ,matumizi ya bangi moja kwa moja?

Vita dhidi ya mihadarati

Ilikuwa mwaka 2012 ambapo Uruguay, ilipoandika historia kwa kuwa taifa la kwanza duniani kuruhusu matumizi ya bangi kwa minajili ya kujiburudisha. Hatua hiyo, kwa uhalisia, ilikuwa na nia ya kuiwezehsa serikali kushughulikia biashara haramu na magenge ya wahalifu waliokuwa wanaiongoza biashara hiyo.

Baadaye mwaka huo, wapiga kura katika majimbo mawili ya Washington na Colorado, wakawa wa kwanza kabisa nchini Marekani kuunga mkono uidhinishwaji wa matumizi ya bangi ambayo si ya kimatibabu.Chini ya utawala wa Barack Obama, msisitizo uliwekwa kwenye majimbo kuwa huru katika kubadili sheria zake za kuratibu matumizi ya bangi.

Majimbo manane mengine kwa pamoja na Washington DC, yameunga mkono uhalalishwaji wa bangi kwa njia ya kujiburudisha huku hukumu ya kupatikana au kutumia kama dawa ikilegezwa kwingineko.

Matumizi ya bangi kwa minajili ya dawa, sasa yanakubaliwa katika majimbo 33 kati ya majimbo 50 nchini Marekani.Sasa wimbi hilo limetanda kote Marekani na linakwenda kwa kasi mno, huku Canada ikihalalisha uuzaji, umiliki na matumizi ya bangi kwa njia ya kujiburudisha kote nchini humo mwezi Oktoba mwaka huu.

Kwa Mexico kuhalalisha bangi bila shaka ni jambo la hakika. Serikali mpya ya Andrés Manuel López Obrador imewasilisha muswada bungeni, ambao utahalalisha matumizi yake kama dawa na burudani, ilihali mahakama ya juu zaidi nchini humo, hivi majuzi iliamua kuwepo kwa marufuku ya matumizi ya bangi kwa njia ya burudani, kwamba ni kinyume cha sheria.

Mataifa mengine yanaongeza shinikizo. Ingawa uuzaji wa bangi unasalia kuwa haramu, kupatikana na kiwango kidogo sio tena uvunjaji wa sheria katika mataifa ya Brazil, Jamaica na Ureno.

Nchini Uhispania ni ruhusa kuvuta bangi japo kwa siri, ilihali dawa hizo zinauzwa wazi katika maduka yenye majina Coffee Shops nchini Uholanzi. Bado mataifa mengi yanakubalia matumizi ya cannabis kwa matibabu.

Nchini Uingereza, madaktari wamekubaliwa kuwapa wagonjwa bidhaa za cannabis tangu mwezi Novemba.Korea Kusini wamehalalisha matumizi ya bangi kama dawa lakini chini ya mazingira yenye sheria kali, licha ya kuwahukumu wakaazi wanaotumia dawa hizo hata nje ya nchi.




Hivyo makala Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?

yaani makala yote Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi? mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/kwa-nini-mataifa-mengi-yameanza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Kwa nini mataifa mengi yameanza kuidhinisha matumizi ya bangi?"

Post a Comment