title : WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO
kiungo : WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO
WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO
Wananchi wameshauriwa kuchunguza afya zao kabla ya kujihusisha na michezo au mazoezi mbalimbali ya viungo vya mwili ili kuepukana na mstuko wa moyo unaoweza kusababisha vifo vya ghafla.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu vifo vya ghafla vinavyowatokea wanamichezo wawapo uwanjani na wananchi wakati wa kufanya mazoezi ya viungo vya mwili.
Prof. Janabi ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema mshtuko wa moyo huufanya moyo kuacha kufanya kazi inavyotakiwa na hii humtokea mtu ambaye mfumo wake wa umeme wa moyo haufanyi kazi vizuri au mishipa ya damu ya moyo imeziba.
Mtu mwingine ambaye hukutwa na tatizo hili ni yule ambaye ana tundu kwenye moyo, mishipa ya damu ya moyo kuwa na matatizo na hivyo kuchanganya damu safi na chafu.
“Jamii yetu imekuwa na tabia ya kufanya mazoezi mbalimbali bila kupima afya ya moyo. Mazoezi yoyote yale ya viungo vya mwili husababisha misuli kujijenga na kuwa mikubwa kama mtu ana ugonjwa wa moyo na misuli yake imekuwa kutokana na mazoezi hupelekea kuziba kwa njia ya damu kutoka kwenye moyo na kusababisha vifo vya ghafla”, alisema Prof. Janabi.
Aidha Prof. Janabi ameviomba vyama vya michezo kushirikiana na hospitali kubwa hapa nchini ili wakati wa michuano mbalimbali itakapotokea mchezaji kupata tatizo la mshtuko wa moyo awapo uwanjani hospitali hizo ziweze kumuhudumia kwa wakati na kuokoa maisha yake.
Kwa upande wa vilabu vya michezo alivihimiza kufanya uchunguzi wa afya ikiwemo afya ya moyo kwa wachezaji wao kabla ya kuwasajili ili kuepuka kutumia fedha nyingi kusajili wachezaji ambao wana matatizo ya kiafya.
Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI )
Hivyo makala WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO
yaani makala yote WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wananchi-washauriwa-kupima-afya-zao.html
0 Response to "WANANCHI WASHAURIWA KUPIMA AFYA ZAO KABLA YA KUJIHUSISHA NA MICHEZO"
Post a Comment