title : UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO
kiungo : UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO
UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Yusuf Ali maarufu kwa jina la ‘Mpemba wa Magufuli',
umetakiwa Desemba 18 mwaka huu kutoa majibu ya kueleweka kuhusu upelelezi dhidi ya kesi hiyo umefikia wapi.Katika kesi hiyo, Yusuph na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.milioni 785.6 milioni. Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu amesema hayo leo Desemba 5, 2018 baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika."Nawapa nafasi ya mwisho upande wa mashtaka hadi Desemba 18. Nataka mje na majibu upelelezi wa kesi hii umefikia kwenye hatua gani? Haiwezekani ichukue muda mrefu kukamilika upelelezi,” amesema Hakimu Simba.
Mapema, Wakili wa Serikali Elia Athanas alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikwenda kwa ajili ya kutajwa na kwamba uandaaji wa nyaraka zote ambazo ni uendeshaji wa shauri pamoja na uchujaji wa washtakiwa upo katika hatua nzuri.
Kutokana na maelezo hayo Wakili wa utetezi Aloyce Komba alihoji ni nyaraka gani hizo na zimefikia hatua gani. Akijibu, Athanas amesema ni nyaraka za uendeshaji na usikilizaji wa shauri hilo pamoja na uchujaji wa washtakiwa kabla ya kuwasomwa maelezo ya mashahidi na vielelezo.
Kesi hiyo imeahirishwakesi hadi Desemba 18 mwaka huu itakapotajwa tena. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, katika tarehe tofauti kati ya Januari 2014 na Oktoba, 2016 wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, washtakiwa wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh.milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa wanyamapori.
Katika shtaka la pili inadaiwa kuwa Oktoba 26, 2016 wakiwa Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam walikutwa na vipande 10 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 13.85 vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 30,000 (Sh 65.4 milioni ). Oktoba 27, 2016 wakiwa Tabata Kisukuru washtakiwa hao wanadaiwa walikutwa na vipande vinne meno ya tembo vyenye uzito wa
kilo 11.1 vikiwa na thamani ya Dola za Marekani 15,000 (Sh 32.7 milioni).
Pia inadaiwa Oktoba 29, 2016 walikutwa na vipande 36 vyenye thamani ya Sh294.6 milioni bila kuwa na kibali cha mkurugenzi wa Wanyamapori.
Hivyo makala UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO
yaani makala yote UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/upande-wa-mashtaka-umetakiwa-kutoa.html
0 Response to "UPANDE WA MASHTAKA UMETAKIWA KUTOA MAJIBU YANAYOELEWEKA KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI YUSUF ALI, WENZAKE WATANO"
Post a Comment