ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI

ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI
kiungo : ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI

soma pia


ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI


Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamiii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amempa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara mwezi mmoja wa kuandaa miundombinu ya wafugaji wa vijiji,Vilima Vitatu,Minjingu waliohamishwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Burunge.

Ulega amesema Mkurugenzi huyo Hamis Malinga anapaswa kuandaa miundombinu hiyo ya wafugaji ili wakiondolewa kwenye hifadhi ya jamii ya Burunge waweze kuhamia Mfulang'ombe kwenye eneo lililojengwa.

Amesema wafugaji hao wanapaswa kuwekewa miundombinu rafiki ikiwemo malambo na majosho ili waweze kuanza maisha mapya ya ufugaji. Amesema wafugaji hao walikuwa wanalalamikia kuondolewa kwenye eneo hilo na kupelekwa sehemu nyingine ambayo haina miundombinu rafiki.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Babati, Hamis Malinga amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa wapo kwenye mchakato wa kuandaa miundombinu rafiki ya wafugaji hao. "Kila mfugaji atapatiwa ekari tatu kwa ajili ya kuhakikisha anazimiliki na tutaandaa malambo na majosho kwa ajili ya mifugo ya hizo kaya 17 zilizoondolewa kwenye hifadhi," amesema.

Kwa muda mrefu kaya 17 za wafugaji wa jamii ya kifugaji ya wabarbaig waliamriwa kuondoka kwenye eneo hilo lakini waligoma.

Eneo la jamii la hifadhi ya wanyamapori Burunge lenye ukubwa wa kilomita za mraba 283 linaundwa na vijiji 10 vya Sangaiwe, Mwada, Ngoley, Vilima Vitatu, Minjingu, Kakoi, Olasiti, Manyara, Magara na Maweni. 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Minjingu na Vilima Vitatu wilaya ya Babati mkoani Manyara ,katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Babati mkoa Manyara wakiangalia hifadhi ya jamii ya Burunge.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwasikiliza wafugaji wa wilaya ya Babati mkoa Manyara walipokuwa wakiwasilisha changamoto zao.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa mkoa wa Manyara katika ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji na wavuvi na kuzitafutia ufumbusi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)


Hivyo makala ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI

yaani makala yote ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/ulega-ampa-mwezi-mmoja-mkurugenzi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ULEGA AMPA MWEZI MMOJA MKURUGENZI HALMASHAURI WILAYA YA BABATI KUANDAA MIUNDOMBINU YA WAFUGAJI"

Post a Comment