title : UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA
kiungo : UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA
UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amefanya ziara ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi kwa wananchi waishio kwenye Mkoa wa Kaskazini kisiwani Pemba na kubaini kuwa yapo baadhi ya maeneo yana usikivu mdogo wa mawasiliano na mengine hakuna kabisa mawasiliano ya simu za mkononi
Nditiye aliambatana na Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah ambaye ndiye chimbuko la ziara hiyo kwa kuuliza maswali Bungeni wakati wa vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu changamoto ya mawasiliano kisiwani Pemba.
“Zipo changamoto mbali mbali ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, wananchi wanapata tabu za kuwasiliana hasa nyakati za usiku hasa wakipata msiba au mgonjwa, tuliwasilisha changamoto hizi Bungeni ili ziweze kutekelezwa,” amesema Maida
Nditiye amebaini uwepo wa usikivu mdogo wa mawasiliano na ukosefu wa mawasiliano wakati wa ziara yake kwenye Shehia ya Kiungoni – Wingwi, Dodeani, Kiuyu Mbuyuni, Sizini – Chwaka, Tumbe, Kipande Konge na Makangale – Mnarani zilizopo kwenye Wilaya ya Micheweni pamoja na kwenye Shehia nyingine za Weni – Tungamaa – Machwengwe, Mtambwe, Mkanjuni na Kivumoni zilizopo kwenye Wilaya ya Wete
“Kuna maeneo ambayo minara ipo ila mawasiliano hayana nguvu na sehemu nyingine hakuna mawasiliano kabisa kutokana na jiografia ya Pemba, nimekuja na wataalamu wa kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), nimewaelekeza hili walifanyie kazi, raha yangu ni kuona wananchi wote wana wasiliana,” amesema Nditiye
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akiwasili kisiwani Pemba kukagua changamoto za mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah na wa kwanza kushoto ni Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Baucha
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyenyoosha mkono) akijadiliana na Shehia wa Sheha ya Kiungoni, Omari Khamisi Othman kuhusu eneo la kujenga mnara wa mawasiliano katika ziara yake ya kukagua changamoto za mawasiliano Pemba. Aliyevaa miwani akisikiliza kwa makini ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akiwa kwenye boti eneo la Makangale – Mnarani akikagua upatikanaji wa mawasiliano wakati wa ziara yake Pemba. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maida Hamad Abdallah na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Mhandisi Peter Ulanga
Hivyo makala UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA
yaani makala yote UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/ucsaf-kupeleka-mawasiliano-ya-uhakika.html
0 Response to "UCSAF KUPELEKA MAWASILIANO YA UHAKIKA KWA WANACHI WA PEMBA"
Post a Comment