title : TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU
kiungo : TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU
TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU
Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amekiri shirikisho hilo kuwa na majadiliano mbalimbali katika ngazi ya Utatu na Upili yaani Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kuhusu hoja ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi za jamii nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari mjini Morogoro leo sanjari na vikao vyao vya kikatiba takribani kwa siku mbili, Nyamhokya amesema wajumbe wamekuwa na fursa ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Ustawi wa Wafanyakazi nchini pamoja na kutoa tamko baada ya kuhudhuria kikao hicho rasmi cha utendaji wa maswala yanayotakiwa kufanyiwa utekelezaji.
Moja ya agenda zilizojadiliwa kwa undani ni swala la uunganiswaji wa wa mifuko ya hifadhi ya jamii na mkanganyiko uliojitokeza baada ya serikali kutangaza kuanza kutumika kwa vikokotoo vya mafao ya pensheni kwa wastaafu wa mifuko ya PSSSF na NSSF kuanzia Agosti 8 2018.
Rais wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya akizungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tannzania. Kushoto ni Makamu Rais wa TUCTA, Qambos Sulle, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Dk Yahya Msigwa (wa pili kulia) na Naibu Katibu Mkuu Jones Majura.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakimsikiliza Rais wa shirikisho hilo, Tumaini Nyamhokya alipozungumza na wanahabari mjini Morogoro leo, wakati wa kutoa tamko la Kamati ya TUCTA Taifa kuhusu mkanganyiko wa kikotoo cha mafao ya pensheni yatolewayo na mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), wakiimba wimbo wa 'Solidarity Forever' wakati wa mkutano huo.
Hivyo makala TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU
yaani makala yote TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tucta-yakiri-kushirikishwa-kwenye.html
0 Response to "TUCTA YAKIRI KUSHIRIKISHWA KWENYE MCHAKATO WA UTUNGWAJI WA KANUNI ZA MALIPO YA WASTAAFU"
Post a Comment