title : WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI
kiungo : WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI
WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Dodoma
Jamii imetakiwa kuacha kabisa tabia ya kuozesha watoto wadogo ambao awajafikia umri wa kuolewa na matokeo yake wawezeshe kupata elimu hili iweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadae .
hayo yamesemwa na Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Vilabu hivyo na wajumbe wa ulinzi wa Mtoto CPT wakati alipokuwa akifanya Tathmini ya mradi huo katika kata ya Kigwe.
"ifike wakati tuone umuhimu wa watoto wetu hasa wakike kuendelea na shule kuliko kuwaozesha ama kuwakimbiza mijini wakafanye kazi za ndani kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kusaidia jamii kuwa endelevu kwa kuwa na wasomi wengi amabo wataweza kujikomboa na kukomboa jamii nzima inayowazunguka kutokana na kile walichokipata " amesea Shao.
Shao aliwasisitiza wajumbe hao wa CPT na Msichana Cafe kuwa makini na kuwaripoti wale wote watakao jiusisha na suala la kuwakatiza watoto shule na kuwapeleka mjini kufanya kazi ama kuwaozesha katika umri mdogo kwa lengo la kuweza kujipatia mali .
alitaja kuwa Msichana Initiative kwa kushirikiana na jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia itawachukulia hatua wale wote ambao watajihusisha na vitendo vya kuwakatiza watoto masomo kwa namna moja ama nyingine ama kuwaozesha wakiwa katika umri mdogo.
Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, akizungumza na moja ya wajumbe wa Msichana Cafe ya Kata ya Kigwe wilayani humo juu ya nini cha kufanya katika kuhakikisha wanaripoti kwa usahii habari za ukatili wa kijinsia na kuwafichua wale wote wanaojiusisha na kuozesha watoto katika umri mdogo hili wasendelee na shule.
Meneja Mradi wa wa Msichana Cafe unaoendeshwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya Msichana Initiative, Sarah Beda akizungumza na wajumbe wa Msichana Cafe na Wajumbe wa CPT Juu ya umuhimu wa kuendelea kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia wanayofanyiwa watoto wa kike katika Kata ya Kigwe ambayo ni moja ya kata kumi zilizo katika Wilaya ya Bahi zinazonufaika na mradi wa Msichana Cafe kutoka Tasisi yake.
Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, akimuelekeza jambo mjumbe wa Msichana Cafe namna ya kujaza fomu ya Tathmini juu ya mradi unavyokwenda katika kata yao.
Meneja Mradi wa wa Msichana Cafe unaoendeshwa na Tasisi isiyo ya Kiserikali ya Msichana Initiative, Sarah Beda akitoa maelezo ya namna ya kujaz afomu za Tathmini ya mradi kwa wajumbe wa Msichana Cafe.
Wajumbe wa CPT wakijaza fomu za Tathmini juu ya Tasisi ya Msichana Initiative ilivyoweza kuasadia katika kufanya kazi zao za kumlinda mtoto katika kata yao na Wilaya ya Bahi.
Wajumbe wa Msichana Cafe wakisikiliza kwa Makini Maelezo yanayotolewa na Dada Sarah Beda ambaye ani meneja mradi huo (ayupo Pichani) juu ya umuhimu wa wao kuongeza juhudi ya mapambano ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Msimamizi wa mradi wa kupinga ndoa za Utotoni na huduma ya Msichana Cafe inayoendeshwa na Tasisi ya Msichana Initiative katika Kata kumi za Wilaya ya Bahi, Francis Eugene Shao, akizungumza na wajumbe wa Msichana Cafe umuhimu wa kutioa taharifa za Ukatili wa kijinsia katika kituo cha Polisi kupitia Dawati la Jinsia hili waweze kupata Msaada kwa haraka.
Hivyo makala WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI
yaani makala yote WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/wakazi-wa-wilaya-ya-bahi-mkoani-dodoma.html
0 Response to "WAKAZI WA WILAYA YA BAHI MKOANI DODOMA WATAKIWA KUWARIPOTI WALE WOTE WATAKAO JIHUSISHA NA KUWAOZESHA WANFUNZI"
Post a Comment