TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa

TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa
kiungo : TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa

soma pia


TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mafanikio hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Fimbo, alisema kuwa TFDA imepata mafanikio hayo makubwa kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, ambapo Desemba mwaka huu, imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imesaidia Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia hatua hiyo muhimu.

“Hii ni hatua kubwa kwa kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuvutia nchi mbalimbali kuja TFDA kujifunza mifumo iliyopo na kwenda kuitekeleza nchini mwao na sasa mifumo yetu imetambulika na kujulikana na nchi nyingi kwa mfano Zimbabwe, Rwanda, Kenya, Uganda, Ethiopia, Sudan Kusini, Botswana, Mauritius, Lesotho na Bangladesh” alisema Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA

Sambamba na hilo, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka ambapo idadi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi vilizosajiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka,

Akitolea mfano katika kipindi cha 2015/16 hadi 2017/18, TFDA imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la 62%. Ikiwa ni kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa TFDA, alifafanua kuwa tathmini na usajili wa bidhaa hufanyika kwa lengo la kuhakiki endapo bidhaa zinakidhi vigezo vya usalama, ubora na ufanisi kabla ya kuruhusiwa katika soko. Kuwepo kwa bidhaa nyingi zilizosajiliwa katika soko ni uthibitisho kuwa walaji wanapata bidhaa zilizo salama, zenye ubora na ufanisi.




Hivyo makala TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa

yaani makala yote TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/tfda-yaongoza-afrika-kwa-kuwa-na-mfumo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TFDA yaongoza Afrika kwa kuwa na mfumo bora wa udhibiti wa dawa"

Post a Comment