Shilawadu ndani ya DStv

Shilawadu ndani ya DStv - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shilawadu ndani ya DStv, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shilawadu ndani ya DStv
kiungo : Shilawadu ndani ya DStv

soma pia


Shilawadu ndani ya DStv

Hatimaye kipindi maarufu cha Shilawadu kuanza kuonekana live ndani ya DStv kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo (DSTV160) kuanzia Ijumaa Desemba 14, 2018. Shilawadu Xtra itaruka hewani kila siku ya Ijumaa saa moja jioni na kurudiwa siku za Jumapili muda huo huo.

Akitambulisha rasmi wa kipindi hicho, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema kuwa kipindi cha Shilawadu Xtra kimeongezwa ladha kadha wa kadha tofauti na awali  na kitagawanyika katika sehemu tofauti tofauti ikiwamo Chemba la Msengenyo, Ubuyu wenye Vitamin Xtra, Kiti cha Moto na Mikikimikiki ya mastaa  ili kuwapatia wateja wa DStv na watazamaji kwa ujumla burudani isiyo kifani .

Amesema kuwa watazamaji wa Maisha Magic Bongo na wapenzi wa Shilawadu hasa wale wapenzi wa umbea wakae mkao wa kula kwani kwa sasa wataweza kushuhudia visa na matukio yote yanayojiri hapa mjini kupitia Shilawadu Xtra chini ya makamanda mahiri wa kipindi hicho akiwemo mkali wa kunyapianyapia Soudy Brown sambamba na kamanda Kwisa ‘Mzee mti mkavu’.

“DStv kupitia Chaneli yake pendwa ya Maisha Magic Bongo(MMB), siku zote tunafanya jitihada kuhakikisha kuwa tunatoa kipaumbele na kuunga mkono maudhui ya ndani na kipindi hiki ni muendelezo wa jitihada hizo”, alisema Alpha.

Kipindi hiki kitakuwa kikiruka hewani kila siku ya Ijumaa saa moja hadi saa mbili usiku na kurudiwa kila Jumapili kwa muda huo huo. Hii itawapa fursa mashabiki na watazamaji wa Maisha Magic Bongo kupata burudani zaidi na haswa kwa wale ambao hawataweza kukitazama kwa siku ya Ijumaa.




Hivyo makala Shilawadu ndani ya DStv

yaani makala yote Shilawadu ndani ya DStv Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shilawadu ndani ya DStv mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/shilawadu-ndani-ya-dstv.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Shilawadu ndani ya DStv"

Post a Comment