title : SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA
kiungo : SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA
SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameitaka Serikali ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha inahusisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA katika ujenzi wa Chuo cha VETA Simanjiro ili miundombinu ya chuo hicho iweze kujengwa kwa utaratibu na viwango vinavyohitajika.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo Mkoani Manyara wakati akikagua eneo ambalo Serikali ya Wilaya hiyo inategemea kujenga Chuo cha Veta kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Hiari ECLAT.
Alisema ni vizuri Mamlaka husika zikahusishwa katika ujenzi wa Chuo hicho tangu hatua za awali na kumtaka Mkurugenzi wa VETA kanda na yule wa Mkoa kufika katika eneo la Emboreet ambako mradi utajengwa kwa lengo la kuongea na wananchi pamoja na wafadhili wa mradi huo ili wazo ambalo limeanza liweze kutekelezwa kwa utaratibu unaostahili.
“Ninyi Halmashauri mnataka kujenga chuo cha Ufundi ni wazo zuri lakini ni lazima kijengwe kwa utaratibu sio kiholela kwa sababu vilianza kuibuka vyuo ambavyo mtu anakuwa na jengo moja anasajili kinaitwa chuo, kuna viwango na masharti ambayo ni lazima yatimizwe kabla chuo kuruhusiwa kufanya kazi, fuateni taratibu hizo ili muweze kuanzisha chuo cha Ufundi,” aliongeza Naibu Wazizri Ole Nasha.

Naibu Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi kuhusu namna walivyojipanga kujenga Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya katika eneo la Mradi la Emboreet lililoko katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kitwai A aliyefanya vizuri katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2018. Shule ya Msingi Kitwai A imefaulisha wanafunzi 25 kati ya 28 waliofanya mtihani mwaka huu.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wakazi wa Kata ya Kitwai A iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo amewataka kuhakikisha wanaandikisha shule wanafunzi wote wenye umri wa kuanza shule bila kuwaacha nyumbani na kuwapangia majukumu mengine.

Hivyo makala SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA
yaani makala yote SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/serikali-wilaya-ya-simanjiro-yatakiwa.html
0 Response to "SERIKALI WILAYA YA SIMANJIRO YATAKIWA KUFUATA UTARATIBU UJENZI WA CHUO CHA VETA"
Post a Comment