title : RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO
kiungo : RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO
RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo, ambapo amewakabidhi Wakuu wa Wilaya na Maafisa Biashara wa Halmashauri mkoani hapa jumla ya vitambulisho 25,000, vitakavyotolewa kwa wajasiriamali wadogo wenye mauzo pungufu ya milioni nne kwa mwaka.
Akikabidhi vitambulisho hivyo Mtaka amesema vitawasaidia wajasiriamali wadogo kutambuliwa,kuwajengea ujasiri na uthubutu na kuwafanya kunufaika na fursa mbalimbali huku akibainisha kuwa vitachangia pia kuwaibua wajasiriamali wapya mkoani Simiyu.
Ameongeza kuwa Simiyu imejipanga kuwafikia wajasiriamali wote wadogo kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais, huku akiwaonya na kuwatahadharisha wafanyabiashara wakubwa wanaotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutojaribu kujipatia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo kwa njia ya udanganyifu.
“Niwatahadharishe wafanyabiashara wasije wakatumia nafasi ya vitambulisho hivi vya wajasirimali wadogo, kufanya udanganyifu wowote wa wao kuvitumia vitambulisho hivyo kujitambulisha kama wafanyabiashara wadogo; huu udanganyifu hatutaupa nafasi na sisi kama Serikali tumejiandaa kuainisha kila mtu anachofanya, mahali anapokaa, historia yake ya biashara”
“Ofisi za Wakurugenzi zitatoa magari yatakayowawezesha maafisa Biashara kwenda vijijini kuwafikia wajasiamali wadogo,tunaamini walengwa wa vitambulisho hivi ni wale ambao nauli ya kule aliko na Makao Makuu ya Wilaya inaweza kuwa ndiyo fedha inayohitajika achangie kupata kitambulisho hicho,kwa hiyo kuna kadi zitabaki wilayani lakini nyingine zitapelekwa mahali walipo walengwa” alifafanua Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka, ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani boksi lenye vitambulisho vya wajasiliamali wadogo, ikiwa ni utekezelaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini, kuwapa vitambulisho hivyo wajasiliamali wadogo ambao mauzo yao ni chini ya milioni nne kwa mwaka ili vitambulisho hivyo viweze kuwafikia wajasiriamali hao mkoani Simiyu.

Hivyo makala RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO
yaani makala yote RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/rc-mtaka-atekeleza-agizo-la-rais.html
0 Response to "RC MTAKA ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, KUWAGAWIA VITAMBULISHO WAJASIRIAMALI WADOGO"
Post a Comment