title : MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA.
kiungo : MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA.
MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA.
Wasanii mbalimbali wakiwa katika majadiliano ya kupinga ukatili ya kijinsia pamoja na rushwa ya ngono.
Kikundi cha wasanii wa filamu wakijadili ukatili wa kijinsia uliopo katika utekelezaji wa majukumu ya kazi yao.
Kikundi cha wasanii wa filamu wakijadili ukatili wa kijinsia uliopo katika utekelezaji wa majukumu ya kazi yao.
Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Agnes Kimwaga (kulia) akizungumza katika warsha ya kupinga ukatili ya kijinsia pamoja na rushwa ya ngono.
Katibu wa Mtandao wa Wasanii Wanawake ambao ni Wanachana wa WFT, Hanifa Sabuni (kushoto) akizumgumza na washiriki wa warsha hiyo kuhusu namna ya kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na rushwa ya ngono katika tasnia ya Sanaa.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam
Wasanii wametakiwa kuwa na ushirikiano katika kupinga ukatili wa kijinsia ikiwemo kuvunja ukimya na kuonesha rushwa ya ngono ambayo imeonekana sio rafiki katika tasnia ya sanaa hapa nchini.
Akizungumza na wada mbalimbali wa sanaa katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Katibu wa Mtandao wa Wasanii Wanawake ambao ni Wanachana wa WFT, Hanifa Sabuni, amesema kuwa kuna ukatili kijinsia unafanyika katika sekta ya sanaa jambo ambalo sio rafiki.
Sabuni amesema kuwa wapo wasanii wengi wanafanyiwa ukatili wa kijinsia bila kujijua kutokana viashiria katika vikundi mbalimbali vya sanaa.
"Hali sio nzuri ndio maana leo tumewaita wasanii na wadau mbalimbali wa sanaa wakiwemo Shirikisho la Filamu Tanzania, vikundi vya music, karakasi, maonyesho ya majukwaa, waandaaji wa music pamoja ufundi" amesema Bi Sabuni.
Hata hivyo Bi Sabuni amebainisha kuwa wametumia warsha hiyo kama sehemu ya kusherekea siku I6 za kupinga rushwa ya ngono kwa wasanii, huku akiwataka wasanii hao kuendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia kazi zao.
Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Agnes Kimwaga, amesema ni vizuri wasanii walioshiriki katika warsha wanapaswa kuwa mabalozi wazuri katika kufikisha ujumbe katika jamii kuhusu mambo yanayotendeka kuhusu ukatili wa kijinsia.
Bi Kamwaga amesema kuwa licha ya kuonekana kwa viashiria vya rushwa ya ngono katika sanaa, lakini mpaka sasa hakuna msanii aliyotoa taarifa kuhusu kufanyiwa ukatili wa kijinsia.
"Ni vigumu kusema moja kwa moja katika sanaa kuna rushwa ya ngono kutokana bado hatujapokea kesi yoyote mpaka sasa" amesema Bi Kimwaga.
Bi Kimwaga amefafanua kuwa wasanii kutotoa taarifa kuhusu ukatili wa kijinsia inasababishwa na wasanii kuona aibu kutoa taarifa sehemu kwa ajili ya kupata msaada.
Amesema kama wasanii wakiendelea kuwa kimya bila kutoa taarifa kuhusu rushwa ya ngono katika kazi yao, kuna uwezekano mkubwa ukatili huo ukaongezeka.
"Jambo la muhimu wasanii wanatakiwa kutokuwa na hofu kitu ambacho kitawasaidia kupiga hatua katika kupinga ukatili wa kijinsia katika utekelezaji wa majukumu yao" amesema Bi Kimwaga.
Mshiriki wa warsha hiyo Mkurugenzi wa Chief Entertainment Salehe Ally, amesema kuwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya filamu wamekuwa wakikutana ukatili wa kijinsia pamoja na rushwa ya ngono hasa kwa wanawake.
Ally amesema kuwa miongoni mwa ukatili wa kijinsia wanaokutana nao ni kulala sehemu ambayo sio rafiki wakiwa eneo la kazi, kulazimishwa kuigiza filamu ambayo ipo kinyume na maadili, kulazimishwa kufanya ngono pamoja kukosekana na huduma ya kwanza pale mwigizaji anapoumia.
"Wakati mwengine upo sehemu mnaigiza, mnakaa muda mrefu bila kula, mtu anaumia apewi dawa, tunalala sehemu ambayo sio rafiki, ukikosea unaambiwa kwa lugha ambazo nzuri"amesema Ally.
Kwa upande wa sanaa ya muziki nao wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na kile kinachodaiwa kulazimishwa kufanya ngono ili waweze kupewa msaada wa kufanikisha kazi anayofanya.
Imeelezwa kuwa kumekuwa rushwa wakati wa kutoa zawadi kwa wasanii, kuimba nyimbo ambazo zipo kinyume na maadili pamoja na kubebeshwa madawa ya kulevya kwenda nayo nje ya nchi.
Hivyo makala MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA.
yaani makala yote MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mtandao-wa-wasanii-wanawake-waendesha.html
0 Response to "MTANDAO WA WASANII WANAWAKE WAENDESHA WARSHA KUPINGA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA SANAA."
Post a Comment