Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima.
kiungo : Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima.

soma pia


Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua huduma mpya ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. Uzinduzi huo umefanyika katika Makao Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Omari Nundu ambaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya TTCL, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujezi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bwana Waziri Kindamba, Wajumbe wa Bodi  na wafanyakazi wa TTCL.

Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Rais alisema uzinduzi wa huduma ya TTCL PESA ni mwendelezo wa jitihada za Kampuni hiyo kurejea katika nafasi yake ya awali ya kuwa suluhisho la kweli la utoaji huduma za Mawasiliano hapa nchini.
Kuzinduliwa kwa huduma hii ni uthibitisho mwingine kwamba, TTCL inatekeleza kikamilifu maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli ambaye ameelekeza kuwa,  Mashirika yote ya Umma yajiendeshe kwa faida, yatoe gawio Serikalini,  yawahudumie wananchi kwa kiwango cha juu kabisa cha ubora na kwa gharama nafuu” alisema Makamu wa Rais.

Aidha, Makamu wa Rais alisisitiza kwamba TTCL PESA itawezesha wananchi kutuma na kutoa pesa kwa viwango vya chini kabisa kupita mitandao yote, pia itawezesha wananchi kulipia Bill za Umeme (LUKU), Maji, Ving’amuzi na kuwezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vya data vya TTCL.  Aliwataka TTCL  kuendelea kuwa wabunifu zaidi ili waweze kuongeza huduma nyingine kadiri mahitaji na siku zinavyokwenda.

Akijibu kuhusu changamoto zilizotajwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Makamu wa Rais alisema Serikali inazijua na itaendelea kuzipatia majawabu. Hatahivyo aliwataka watumie vyema rasilimali walizopewa ikiwamo Mkongo wa Taifa na Kituo cha Kuhifadhia Kumbukumbu za kimtandao kupata pesa za kujiendeshea.

Makamu wa Rais pia aliipongeza menejimenti ya TTCL kwa wazo lao la kufikiria kuanzisha kiwanda cha simu hapa nchini.  Alisema “msisitizo wa serikali yetu kwa sasa ni ujenzi wa uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025 kupitia uwekezaji katika viwanda hivyo wazo lenu la ujenzi wa kiwanda cha simu limekuja wakati muafaka”.

Mwisho, Makamu wa Rais alisema TTCL PESA itatoa fursa kubwa ya ajira kwa wananchi kuwa mawakala na  itarahisisha shughuli za kiuchumi hasa biashara na hivyo aliwasihi wananchi kuonesha uzalendo wao kwa kutumia huduma za TTCL.

Baada ya uzinduzi huo Makamu wa Rais alishiriki katika Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Linah George Mwakyembe ambaye ni mke wa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo iliyofanyika katika kanisa la KKKT Kunduchi Beach, Dar es Salaam.


Hivyo makala Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima.

yaani makala yote Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/makamu-wa-rais-mhe-samia-suluhu-azindua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Azindua TTCL Pesa na Kutoa Heshima."

Post a Comment