title : MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE
kiungo : MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE
MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
MSANII nguli nchini kwenye tasnia ya filamu ya maigizo Hashim Kambi ahimiza nidhamu iwe ni kipaumbele kwa wasanii wenye majina maarufu pamoja na chipukizi katika kukuza tasnia hiyo.
Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumzia mienendo ya baadhi ya wasanii ambapo amesema hairidhishi na inasababisha wasanii kutopata nafasi kwenye masoko ya nje huku akitolea mfano nchi jirani kama ya Kenya.
Kambi amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya wasanii wa Tanzania na Kenya ambapo, wasanii wa nchi hiyo wanazingatia nidhamu kwa kiwango cha hali ya juu bila kujali ukubwa au udogo wa jina na wanaheshimiana katika kazi zao za sanaa.
Pia amesema wasanii wenye majina huwapa kipaumbele wasanii wakongwe ambao ambao wapo kwenye tasnia kwa muda mrefu na kuona ni fursa adhim kwa wakongwe hao kuendelea kutoa mafunzo na ujuzi ili kuleta mapinduzi katika sekta ya filamu nchini.
Kuhusu sanaa yake ya uigizaji wa filamu , Kambi amesema kwa sasa ameshiriki kwenye filamu ya hukumu ya Msanii Rammy ambayo inalenga kutoa elimu kwa jamii kuhusu janga la dawa ya kulevya ambalo linaonekana kushamiri na kusababisha athari kwa vijana wengi nchini.
Msanii wa nguli wa filamu hapa nchini Hashim Kambi akizungumza na wanahabari kuhusu uzinduzi wa filamu ya Rammy Garis inayoitwa hukumu yangu leo Jijini Dar es Salaam , iitakayozinduliwa Desemba 15 mwaka huu katika moja ya ukumbi uliyopo City mall.
Hivyo makala MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE
yaani makala yote MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/msanii-nguli-wa-filamu-za-kibongo.html
0 Response to "MSANII NGULI WA FILAMU ZA KIBONGO HASHIM KAMBI AHIMIZA NIDHAMU KWA WASANII WOTE"
Post a Comment