Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro

Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro
kiungo : Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro

soma pia


Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro

Zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi inayotolewa katika kampeni inayoendelea ya Tigo Jigiftishe, ilikabidhiwa mwishoni mwa wiki kwa Flora Somba ambaye ni mkazi mjini Morogoro . 

Flora anakuwa ni mshindi wa nne kupata zawadi ya shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es Salaama pamoja na Mbwana Mbela mkazi wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma. Akiongea huku akibubujikwa na machozi wakati akikabidhiwa zawadi yake, Flora ambaye anafanya kazi za vibarua kwenye ujenzi kama kubeba zege, alisema Mungu amemtendea miujiza kupitia Tigo Jigiftishe. 

“Nalea watoto wawili peke yangu, mimi ndiyo baba na mimi ndiyo mama. Binti yangu Irene alilazimika kuacha shule kwa sababu sikiuweza kumlipia ada, nashukuru Mungu sasa ataweza kurudi shuleni,asante Tigo kwa kubadilisha naisha yangu” alisema .Flora alisema fedha atakazopata pamoja na kusaidia ada za watoto, atajitahidi kujenga nyumba walau ya vyumba viwili ili kuachana na nyumba za kupanga na kuongeza kuwa fedha itakayobaki atafungua biashara itakayomsaidia kuhudumia familia yake. 

Hafla ya kukabidhi mshindi wa milioni 10 zawadi yake, ilienda sambamba na kuwakabidhi washindi wengine saba wa shilling milioni moja moja kutoka mkoa wa Morogoro zawadi zao .Akiongea wakaati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Tigo kwa Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema promosheni ya Jigiftishe inalenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za mtandao huo katika kipindi hiki cha sikukuu. 
 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro (wa kwanza kushoto) akiwa na uso wa furaha na binti yake Irene Hatibu (wa pili kushoto) muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake.  Wa kwanza kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa. Wengine ni Viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani.

 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro akijifuta machozi  ya furaha muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake mjini Morogoro mwishoni mwa wiki. Kulia ni mtangazaji wa Radio Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo kanda ya Pwani.

 Mshindi wa zawadi ya shilingi milioni 10 ya Tigo Jigiftishe Flora Somba  kutoka Morogoro (wa tatu kulia), akiwa na washindi wa shilingi milioni moja moja kutoka mkoani Morogoro muda mfupi baada ya wote kukabidhiwa zawadi zao. Kulia ni mtangazaji wa Clouds FM Mina Ally na wengine ni viongozi wa Tigo Kanda ya Pwani.



Hivyo makala Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro

yaani makala yote Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/milioni-10-za-tigo-jigiftishe-zaenda_17.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda Morogoro"

Post a Comment