title : MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI
kiungo : MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI
MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI
*Aagiza wakae na wakandarasi wao na kupima kama watamaliza kazi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la tenki la maji la kutolea huduma katika ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba badala ya ukumbi wa Hazina kama alivyokuwa amepanga awali.
Akiwa Ihumwa, Waziri Mkuu amewaagiza Mawaziri wafike kwenye maeneo ya ujenzi wa ofisi zao, watathmini uwezo wa wakandarasi wanaojenga majengo ya wizara na pale watakapojiridhisha kuwa uwezo wao ni mdogo, wawabadilishe mara moja.
Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Desemba 28, 2018) akiwa kwenye kikao cha kazi (site meeting) na mawaziri 15 na manaibu mawaziri katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.“Mawaziri mliopo na makatibu wakuu wote kaeni na wakandarasi wenu hapa site ili waeleze kazi hii itakamilishwa lini. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kazi hii inakamilishwa kwa wakati,” amesisitiza.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa mrejesho Mawaziri juu ya changamoto alizokutana nazo jana alipofanya ukaguzi wa ujenzi kwa kila wizara. “Nataka Mawaziri ambao ofisi zao zinajengwa wa watu wa Mzinga, wakae nao na kutathmini uwezo wao na kama mtaona hawawezi, mkabidhi kwa mkandarasi mwingine,” amesema Waziri Mkuu.
Amewataka wakandarasi wahakikishe wanaongeza idadi ya vibarua ili kazi hiyo iweze kwenda haraka. “Wizara iliyofanya vizuri kuliko zote ni ya Utumishi, wao wako hatua nzuri. Kwa maana ya uchapaji kazi, eneo nililokuta lina wafanyakazi wengi ni magereza,” amesema.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma, unapojengwa Mji wa Serikali kukutana na Mawaziri na Makatibu Wakuu, Desemba 28, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango na kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa mji wa Serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dkt. Maulid Banyani baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa Mji wa Serikali, Desemba 28, 2018. Katikati ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi baada ya kuzungumza na Mawaziri na Makatibu Wakuu kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma unapojengwa mji wa serikali, Desemba 28, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Hivyo makala MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI
yaani makala yote MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/majaliwa-akutana-na-mawaziri-eneo-la.html
0 Response to "MAJALIWA AKUTANA NA MAWAZIRI ENEO LA IHUMWA DODOMA UNAPOJENGWA MJI WA SERIKALI"
Post a Comment