title : MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO.
kiungo : MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO.
MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO.
Hayo yamebainishwa na Afisa kilimo wa Manispaa ya Kinondoni Ndg. Salehe Hija, ambaye pia ni msimamizi wa kituo cha kilimo malolo alipokuwa akifunga mafunzo ya kilimo yaliyoendeshwa kwa siku tano kituoni hapo yenye lengo la kuwapa ujuzi wakulima wa jinsi ya kulima kilimo hai bila matumizi ya kemikali.
Amesema wakulima wengi wa mbogamboga hupenda kutumia kemikali katika mazo yao hali inayopelekea kilimochao hicho kuwa duni na wakati mwingine kushindwa kukabiliana nacho.
"Hapo nyuma uliwahi kufanyika utafiti ambao ulibaini kwamba changamoto nyingi ambazo wakulima hawa wa mbogamboga wanakutana nazo, hasa hiki kilimo cha mjini, ni matumizi ya kemikali na ikaonekana njia pekee ya kuondokana nazo ni kuwapa mafunzo ya utaalam huo" Amefafanua Hija.
Aidha Ndg Hija amewataka wakulima waliopatiwa mafunzo hayo kuwa chachu ya mabadiliko kwa wakulima wengine katika maeneo yao, kwa kuwafundisha kwa vitendo njia bora za kilimo na jinsi ya kuongeza tija katika mazao yao, hasa ikizingatiwa sekta ya kilimo ndio msingi imara wa maendeleo kwa Taifa letu.
Naye mtafiti aliebaini changamoto za wakulima zilizopelekea mafunzo hayo Bi Christina Kivunda katika nasaha zake, amewashauri wakulima na wasindikaji wa mazao ya kilimo kujikita kwenye aina moja ya kitu ambacho kufanyika kwake kwa muda mrefu kutakujengea uwezo mzuri na ufanisi katika hicho, hali itakayokufanya kukipenda na kukuletea tija kuliko kuendelea kujaribu aina mbalimbali za kilimo kusikoleta ufanisi.
Kwa nyakati tofauti wakulima hao wa mbogamboga wameushukuru uongozi mzima wa Manispaa ya kinondoni kwa kuwaletea mafunzo hayo, kwani yamewawezesha kujifunza mbinu mbalimbali za utafutaji wa masoko, jinsi ya kuandaa mradi, na jinsi ya kutayarisha mbolea kwa dawa za asili, hali iliyowabadilisha kutoka wakulima wa kawaida na kuwa wakulima wenye tija.
Mafunzo haya ya siku tano yaliyofanyika kituo cha malolo yamefadhiliwa na wadau kutoka Chuo kikuu Cha Dar es salaam, Chuo kikuu Cha Ordenburg cha Ujerumani, Chuo kikuu Cha Nelson Mandela Cha Africa kusini pamoja na Mtafiti Bi.Christina Kivunda.
Imeandaliwa na
Kitengo Cha Habari na Uhusiano
Manispaa ya Kinondoni.
Hivyo makala MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO.
yaani makala yote MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/mafunzo-ya-kilimo-bora-na-hai-ndio.html
0 Response to "MAFUNZO YA KILIMO BORA NA HAI, NDIO MSINGI IMARA KWA WAKULIMA WA MBOGAMBOGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA SEKTA HIYO."
Post a Comment