title : DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO
kiungo : DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO
DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO
Na Bashir Yakub.
Huna haja ya kuvutana na mtu kuhusu iwapo wewe ni baba wa mtoto au hapana. Nimesema baba kwasababu wasiwasi wa aina hii mara zote upo kwa wanaume. Kuwa fulani ni mama wa fulani karibia mara zote hapana utata.
Basi wapo wanaopenda au ambao wangependa kufanya vipimo vya vinasaba(DNA) kuthibitisha kama ni wazazi kweli ama hapana. Nitaeleza utaratibu mzima hapa kutokana na Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba vya Binadamu ya 2009,Sura ya 73.
1. NANI ANAWEZA KUPIMWA DNA.
Yeyote ambaye anahitaji kujua kuhusu uhalali wa uzazi wake anaweza kupima DNA. Upimaji huu hauna umri. Hata hivyo DNA si kwa jili ya masuala ya kuthbitisha uzazi tu, bali hutumika hata katika masuala ya ushahidi na upelelezi.
2. NANI ANA MAMLAKA YA KUOMBA DNA KUPIMWA.
Si kila mtu anaweza kuomba kupima DNA. Hata kama mwenye uhitaji ni wewe lakini bado huna mamlaka ya kuomba kupima DNA. Kifungu cha 25(2) cha Sheria niliyotaja hapo juu kinawataja wafuatao kuwa na mamlaka ya kuomba DNA kupimwa. Kinamtaja hakimu ambapo kuna kesi/shauri fulani linaendelea, Wakili, afisa ustawi wa jamii, afisa polisi mwenye cheo zaidi ya inspector,daktari, na mkuu wa wilaya.Hawa ndio wenye mamlaka(Requesting Authority).Kwahiyo wewe ukiwa na shida ya DNA unaweza kumuona mmoja kati ya hawa ili aandae maombi ya kupima DNA na kuyapeleka kunakostahili.
3. MAOMBI YA DNA YANAPELEKWA WAPI
Kifungu cha 24 cha Sheria ya Usimamizi wa Vinasaba kinaitaja maabara ya Vinasaba vya binadamu ya Mkemia Mkuu wa serikali kuwa na Mamlaka ya kupima DNA. Pia kinazitaja na maabara nyingine ambazo zitakuwa na leseni maalum ya kupima DNA kuwa na mamlaka hayo.
Kwahiyo maombi ya DNA yatapelekwa moja kati ya sehemu hizo mbili.
Hivyo makala DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO
yaani makala yote DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/dna-ujue-utaratibu-wa-kisheria-wa-kujua.html
0 Response to "DNA, UJUE UTARATIBU WA KISHERIA WA KUJUA MTOTO NI WAKO AMA SI WAKO"
Post a Comment