DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII

DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII
kiungo : DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII

soma pia


DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

DROO ya upangwaji wa Makundi hatua ya 16 bora ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF) inatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa Disema 28 ili kupata makundi manne yatakayoanza kuchuana Januari 16 mwaka huu makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.

Timu hizo zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 baada ya kufanikiwa kushinda mechi zao za mzunguko wa pili na kutoka Afrika Mashariki na kati timu pekee kutoka Tanzania Simba wamefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuwafungwa Nkana 'Red Devil' goli 3-1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 2-1 wakiwa ugenini.

Katika uchezeshaji wa droo hiyo timu ya Simba imewekwa katika kundi cha nne kutokana na nafasi ya kisoka kwa klabu za Afrika na watasubiri timu zitakazoanza kupangwa kutoka kundi la kwanza hadi la tatu.Mbali na Simba SC, timu nyingine zilizofuzu Ligi ya Mabingwa Afrika ni mabingwa watetezi, Esperance na Club Africain zote za Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Ismailia, Al Ahly za Misri.

Timu zingine TP Mazembe na AS Vita za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Wydad Casablanca ya Morocco, JS Saoura, CS Constantine za Algeria, Horoya FC ya Guinea, Lobi Stars ya Nigeria, FC Platinums ya Zimbabwe na ASEC Mimosa ya Ivory Coast.

Mara ya mwisho Tanzania kuingiza timu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka 2003 na walikuwa hao hao Simba SC waliofika hatua hiyo, wakifuata nyayo za wapinzani wao wa jadi, Yanga SC waliokuwa timu ya kwanza nchini kufikia mafanikio hayo mwaka 1998. 


Hivyo makala DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII

yaani makala yote DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/droo-ya-makundi-klabu-bingwa-afrika.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DROO YA MAKUNDI KLABU BINGWA AFRIKA KUPANGWA IJUMAA HII"

Post a Comment