title : AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA
kiungo : AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA
AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA
Shirika la Agape la Mjini Shinyanga limefanya Kongamano kwa wanafunzi 400 wa shule za msingi na sekondari katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi na ujinsia ili kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.
Kongamano hilo lililohudhuriwa na wanafunzi wa shule nane zilizopo katika kata hiyo,limefanyika katika Uwanja wa Kijiji cha Singita ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mary Maka.
Wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo ni kutoka shule za msingi Nzagaluba, Manyada, Busanda, Shabuluba pamoja na Shingida ambapo za sekondari ni Samuye, Usanda na Shingita.
Kongamano hilo lililoanza kwa maandamano lilienda sanjari na Mdahalo wenye mada ‘Nini Manufaa/faida ya elimu ya afya ya uzazi na ujinsia’ pia lilitawaliwa na michezo na burudani mbalimbali kutoka kwa wanafunzi hao vyote vikilenga kutokomeza mimba na ndoa za utotoni.
Wanafunzi wa shule mbalimbali katika kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiandamana kuelekea katika uwanja wa kijiji cha Singita kata ya Usanda ambapo pamefanyika kongamano kwa ajili ya kutoa elimu afya ya uzazi na ujinsia ili kutokomeza mimba na ndoa za utotoni. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Afisa mradi wa afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana kutoka Shirika la Agape, Lucy Maganga akielezea lengo la kongamano la wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kata ya Usanda ambalo limelenga kutoa elimu kuhusu afya ya uzazi na ujinsia ili .kukabiliana na mimba na ndoa za utotoni.
Kaimu Afisa Elimu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mary Maka akiwasisitiza wanafunzi/watoto kutoa taarifa kwa viongozi na vyombo vya dola pale wanapofanyiwa vitendo vya kikatili.
Hivyo makala AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA
yaani makala yote AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/agape-yafanya-kongamano-la-elimu-ya.html
0 Response to "AGAPE YAFANYA KONGAMANO LA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UJINSIA SHULE 8 ZA USANDA"
Post a Comment