title : WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF
kiungo : WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF
WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF
Na Lusungu Helela-Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa mradi wa viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda
Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizindua Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo kuwa pamoja na utekelezaji wa maagizo mengine aliyowapatia, suala la uanzishwaji viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali na bidhaa nyingine zitokanazo na ufugaji nyuki katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya liinapaswa kupewa uzito wa juu kiutekelezaji.
Waziri Kigwangala ameongeza kuwa ni azma ya Serikali ya awamu ya tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025 na kuwa suala hilo lina umuhimu mkubwa kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..
Ameongeza kuwa endapo suala hilo la viwanda litafanikiwa , itasaida kuchochea jamii kuwa mstari wa mbele kulinda misitu badala ya sasa jamii kujikita kwenye ukataji miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa jangwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania pamoja na sekretarieti ya Bodi hiyo wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo iliyofanyika jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania, Prof. Romanus Ishengoma akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Romanus Ishengoma mara baada ya Waziri Kigwangalla kuzindua Bodi hiyo jijini Dodoma.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu (kushoto) wakimkabidhi kabrasha Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Misitu Tanzania, Tuli Msuya (kulia) wakati Waziri Kigwangalla alipokuwa akizindua wa Bodi hiyo jijini Dodoma.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Hivyo makala WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF
yaani makala yote WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-kigwangalla-aitega-bodi-ya.html
0 Response to "WAZIRI KIGWANGALLA AITEGA BODI YA WADHAMINI YA TaFF"
Post a Comment