title : Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82.
kiungo : Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82.
Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82.
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) imewahakikishia wakulima kuwa upatikanaji wa mbolea hapa nchini ni wa uhakika na wakulima wasiwe na hofu katika kipindi hiki ambacho msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 unatarajia kuanza.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Lazaro Kitandu alisema kuwa kwa sasa kuna zaidi ya asilimia 82 ya mbolea inayopatikana nchini katika kipindi cha mwanzo wa msimu wa kilimo, hali ambayo itasaidia wakulima kufanya shughuli zao bila wasiwasi.
“Kwa sasa tayari tuna zaidi ya asilimia 82 ya mbolea katika kipindi hiki cha mwanzo wa msimu, na kiasi kingine kilichobaki tunaweza kuagiza kwa sababu muda tunao wa kutosha, na hivyo wakulima wanaweza kuendelea na shuguli za kilimo bila kuhofia upatikanaji wa mbolea “ alisema.
Alifafanua kuwa katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019, makisio ya mahitaji ya mbolea kwa nchi nzima yatakuwa tani 514,138, ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 14 ikilinganishwa na matumizi ya mbolea katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 ambapo mbolea ilikuwa tani 450,000, aidha, hadi kufikia mwezi Novemba 8 mwaka huu jumla ya tani 422,088 za mbolea zilikuwepo nchini, ikiwa ni ni takribani asilimia 82 yamahitaji ya mbolea kwa msimu wa kilimo kwa mwaka 2018/2019.
Aidha, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kuwa,kutokana na mfumo wa sasa wa Serikali ambao unadhibiti uingizaji na usambazaji wa mbolea nchini umesaidia kuwa na kiasi hicho kikubwa cha mbolea kwa mwaka huu.
Aliongeza kuwa, katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 mahitaji ya mbolea za kupandia yaani (DAP) zilizoingizwa kwa mfumo wa ununuzi wambolea kwa pamoja (BPS) zilikuwa tani 80,859. Ambapo hadi kufikia Novemba 7 mwaka huu tayari kulikuwa na jumla ya tani 95,712 za mbolea aina ya DAP hapa nchini, ikiwa ni zaidi ya asilimia 100 ya mahitaji ya mbolea kwa msimu mzima.
Halikadhalika, mbolea inayotengenezwa hapa nchini katika kiwanda cha Minjingu ambayo inatumika kwa ajili ya kupandia na kukuzia mazao tayari imeshasambazwa katika mikoa mbalimbali kiasi cha tani 6,548 .
Upatikanaji wa mbolea nchini umechangiwa kwa kiasi kikubwa na sera wezeshi zilizowekwa na Serikali ikiwa ni pamoja na Mfumo wa Uigizaji wa Mbolea kwa pamoja yaani BPS kwa lengo la kuwa na uhakika wa upatikanaji wa mbolea hapa nchini pamoja na punguzo la bei kwa mkulima.
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea (TFRA) ni taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Kilimo ambayo ina jukumu la kusimamia na kudhibiti utengenezaji,uingizaji na uuzaji wa mbolea hapa nchini.
Hivyo makala Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82.
yaani makala yote Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/upatikanaji-wa-mbolea-nchini-sasa-ni.html
0 Response to "Upatikanaji wa Mbolea Nchini sasa ni Zaidi ya Asilimia 82."
Post a Comment