title : TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO
kiungo : TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO
TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imesema haitasita kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote wanaopotosha jamii na vitendo vya uvunjifu wa maadili ya kitanzania kwa kujirekodi na kisha kusambaza picha za video za utupu mtandaoni.
Akizungumza leo Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA Joannes Karungura amesema kutokana na video inayosambaa kwa sasa nchini ikimuhisha msanii wa filamu nchini Wema Sepetu imeamua kumfikisha mahakamani ili asomewe shtaka linalomkabili na kwamba huo ni mwanzo tu kwani wote ambao wanaokiuka maadili mitandaoni watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Karungura amebainisha kuwa sheria zitaendelea kufuatwa na kwa yoyote atakayekiuka maadili ya kitanzania kama alivofanya Wema
Sepetu na wengine ambao kesi zao ziko Kwenye taratibu kufikishwa
mahakamani basi watatumikia kifungo cha miaka Saba au kutoa faini
ya Sh.millioni saba.
Ametoa mwito kwa Watanzania kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha jamii yetu inakua na maadili,tabia njema pamoja na desturi nzuri ili kukijenga kikazi cha kesho na vinavokuwa maadili mazuri na hofu ya kutokufanya vitendo viovu.
Pia amewataka watu wenye picha pamoja na video chafu kufuta mara
moja kwani TCRA wana mikakati mizito kwa watu ambao wanahifadhi
pamoja na wanaosambaza picha hizo kuwafikisha Kwenye sheria
ichukue mkondo wake.
Hivyo makala TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO
yaani makala yote TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/tcra-yatangaza-kuwachukulia-hatua.html

0 Response to "TCRA YATANGAZA KUWACHUKULIA HATUA WAVUNJIFU WA MAADILI KATIKA MITANDAO"
Post a Comment