title : TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
kiungo : TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
Mkoa wa Tanga unatarajiwa kuwa mwenyeji mazoezi ya mafunzo ya Ushirikiano Imara 2018 ya kijeshi ya vikosi vya Majeshi ya Nchi za Afrika ya Mashariki Kuanzia Novemba 9 hadi 21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari hapo Mkuu wa Mafunzo na Oparesheni (JWTZ) Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga alisema kuwa mafunzo hayo yatalenga katika kujenga uwezo wa kukabiliana na uharibifu pamoja na majanga.
Alisema kuwa dhumuni la zoezi hilo la kikanda ni kubadilishana uzoefu wa kiutendaji ikiwemo kuimarisha mahusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi nyingine. “Kutokana na Oparesheni Matumbawe iliyofanyika mwaka jana kuleta matokeo bora tumeona na awamu hii kuutumia mkoa wa Tanga kwa ajili ya mazoezi hayo ya vikosi “alisema Meja Jenerali Kapinga.
Alisema kuwa mafunzo hayo ambayo yatakuwa ya awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni mafunzo ya ndani yameanza leo mjini hapa wakati awamu ya pili itahusisha mafunzo ya nje yatakayoanza Novemba 9 mwaka huu.Aliongeza kuwa pamoja na mafunzo hayo majeshi hayo yataweza kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwa jamii ya wanatanga kama vile ujenzi wa ofisi ya walimu,na vyoo katika shule ya msingi Machemba iliyoko wilayani Muheza.
Pia alisema kuwa kutakuwa na utoaji wa huduma bure za tiba katika eneo la zoezi kwa wananchi kwa magonjwa mbali hivyo kutumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi ili waweze kupatiwa matibabu. Nae Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigela alisema kuwa vikosi vya majeshi ya nchi za Burundi,Kenya,Uganda na Rwanda tayari vimeshawasili mkoani humo kwa ajili ya maandalizi ya mafunzo hayo.
Alisema kuwa kwa mwaka huu idadi ya wanajeshi 1500 wanatarajia kushiriki katika mafunzo hayo ,kwa kupeana ujuzi na kubadilishana mbinu mbalimbali za kijeshi. “Mazoezi hayo ni fursa nzuri kwa mkoa wetu nah ii inaonyesha ni namna gani mkoa ulivyo katika hali ya usalama ,utulivu na amani ndio maana kwa mara ya pili mafunzo yanaletwa Tanga.
Hivyo makala TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
yaani makala yote TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/tanga-kuwa-mwenyeji-wa-mazoezi-ya.html
0 Response to "TANGA KUWA MWENYEJI WA MAZOEZI YA MAFUNZO YA USHIRIKIANO IMARA 2018 YA KIJESHI YA VIKOSI VYA MAJESHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment