title :
kiungo :
*RC MAKONDA AWAALIKA WANANCHI KUSHUHUDIA TUKIO LA RAIS MAGUFULI KUKABIDHI KOMBE KWA TIMU YA SIMBA*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *Mhe. Paul Makonda* amewahakikishia *usalama mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu* watakaojitokeza kwenye Mechi Kati ya Timu ya *Simba na Kagera Sugar* itakayopigwa kwenye *Uwanja wa Taifa* ambapo Mgeni Rasmi atakuwa *Rais Dr. John Magufuli* ambae atakabidhi kombe la *Ubingwa wa VPL* 2017/2018 kwa Timu ya *Simba.*
*RC Makonda* amesema hayo wakati alipotembelewa ofisini kwake na *viongozi wa timu ya Simba* ambapo amesema kitendo cha *Rais Magufuli* kukubali kuwa *mgeni rasmi* siku ya kesho ni *heshima* kubwa kwenye tasnia ya *michezo* kwakuwa uwepo wake utakuwa na *manufaa makubwa* katika maboresho kwenye *sekta ya michezo.*
Aidha *RC Makonda* amesema anachofurahia ni kuona *Timu ya Simba iliyopo mkoa wa Dar es salaam* inanyakua kombe jambo ambalo ni *heshima kubwa* pia kwa Mkoa.
Kuhusu suala la *msongamano wa magari* barabarani *RC Makonda* amesema watahakikisha hakuna *foleni* ili hata wale *waliofungwa kwaajili ya Ramadhan* waweze kuwahi nyumbani *kufuturu* ambapo amewasihi wananchi *kujitokeza kwa Wingi.*
Hivyo makala
yaani makala yote
Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/05/rc-makonda-awaalika-wananchi-kushuhudia.html
0 Response to " "
Post a Comment