title : Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda
kiungo : Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda
Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda
Hussein Ndubikile
Mwamba wa Habari
Serikali ya Awamu ya Tano imesema imedhamiria kufanya mageuzi katika Sekta ya Kilimo ambapo Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara za Sekta ya Kilimo (ASLMs) na wadau wa kilimo inatekeleza Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDPII).
Katika progaramu hiyo utekelezaji unalenga kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo (mazao, mifugo na uvuvi) ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha na usalama wa chakula na lishe.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati akifungua warsha ya Siku mbili ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania(ACT).
Amesema utekelezaji wa lengo hilo ni kuhakikisha kuwa Taifa linaendelea kujitosheleza kwa chakula; kuimarisha uchumi; kuwa kichocheo cha kukua kwa viwanda; na kuongeza ajira ambapo ili kufikia malengo hayo; Utekelezaji wa ASDP II utazingatia mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
“Tumeanza na mbolea ambapo kwa sasa inaagizwa kwa pamoja na tumeondoa kodi na tozo nyingi katika mbolea ili ipatikane kwa bei nafuu. Kwa sasa changamoto kubwa imebaki kuwa gharama kubwa ya usafirishaji hasa kwa maeneo ambayo hakuna usafiri wa reli ambapo Serikali bado inalifanyia kazi suala hili” Amesema na kuongeza kuwa
“Changamoto nyingine kama nilivyozitaja hapo awali tutaendelea kuzifanyia kazi na tunaomba wadau kupitia vyama vyenu na taasisi kilele kama Baraza la Kilimo, muendelee kutupa maoni yetu ya namna bora ya utatuzi na sisi tunaahidi kufanyia kazi maoni yenu”.
Amebainisha kuwa serikali inatambua changamoto za masoko, usindikaji, miundombinu ya umwagiliaji na miundombinu mingine kwa ajili ya mifugo na uvuvi, upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakati na kwa bei nafuu, uhaba wa maafisa ugani, kero za kodi na tozo mbalimbali, wingi na mwingiliano wa taasisi za udhibiti huku akiahidi kuendelea kuzitafutia ufumbuzi.
“Baadhi ya kero hizi zimeshaanza kufanyiwa kazi. Mifano michache ni kuhusu tozo na kodi ambapo Serikali imeondoa kodi na tozo nyingi katika sekta ya Kilimo na bado tunaendelea kufanya maboresho katika eneo hilo.” amesema
Aidha, alisema kuwa Wizara ya Kilimo inatambua mahusiano ya moja kwa moja kati ya Sekta ya Viwanda na ile ya Kilimo na pia changamoto zilizopo.
“Pamoja na dhamira ya Serikali iliyokuwepo katika kuweka mazingira mazuri ya biashara, ACT kama sehemu ya timu ya Kikosi Kazi Cha Taifa Cha Kuishauri Serikali Kuhusu Masuala ya Kodi, imekuwa ikitekeleza jukumu hilo bila kuchoka ambapo kwa kupitia ushauri huo, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018 na 2018/2019 Serikali imepunguza kodi na tozo nyingi sana katika sekta ya kilimo” Amesisitiza Hasunga.
Ameafafanua kutokana na jitihada hizi za ACT katika kuona kuwa kilimo kinakuwa moja ya ajenda kubwa kitaifa, Serikali kupitia wizara hiyo imekubali kuwa na makubaliano maalumu na ACT kwa lengo la kuifanya sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Warsha ya Wadau wa Baraza la Kilimo na Mifugo imebeba kauli mbiu isemayo “Kilimo na Maendeleo ya Viwanda Tanzania” ambapo wadau wa sekta ya Kilimo katika maeneo mbalimbali ya mnyororo wa thamani yaani kuanzia wazalishaji (wakulima, wafugaji na wavuvi), wasindikaji, watoa huduma mbalimbali kama wasafirishaji na wauza pembejeo, wafanyabiashara ya mazao, wasindikaji ikiwa na mada mbalimbali zenye kuakisi juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuwa na Uchumi wa Viwanda ifikapo 2025.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ACT, Sinare Yusup Sinare amesema warsha hiyo itasaidia wanaushirika kutoa maazimio yatakayosaidia Tanzania kuelekea kwenye uchumi wa viwanda kama ilivyokusudiwa.
Naye, Mwenyekiti wa Wa Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Maziwa mkoani Kilimanjaro, Nancy Manaseh amesema kupitia muungano huo tayari wafugaji 250 wamepata elimu ya upimaji maziwa huku wengine 150 wakinufaika na malisho bora.
Hivyo makala Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda
yaani makala yote Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/serikali-baraza-la-kilimona-mifugo-act.html
0 Response to "Serikali, Baraza la Kilimona Mifugo (ACT) zapania kufanya mageuzi kuelekea Tanzania ya Viwanda"
Post a Comment