title : SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA.
kiungo : SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA.
SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa kituo cha taarifa na Maarifa Sayari Group Nipaeli Mrutu akichanganya udongo na mbolea kwa ajili ya kutumika kuandaa shamba, wengine ni wanachama wa Sayari Group
Wanachama wa Sayari Group wakipalilia mboga mboga walizopanda katika shamba la kisasa.
Shamba la kisasa ambalo limeandaliwa kwa ajili ya kupanda mazao mbalimbali.
Wanachama wa Sayari Group wakiwa shambani.
Shamba la kisasa linalomilikiwa na kikundi cha Ujasiliamali wa Kilimo cha Mboga mboga Sayari Group kilichopo Chanika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa kituo cha taarifa na maarifa Sayari Group Nuru Dilangale akizungumzia maendeleo ya shughuli wanazofanya.
Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Sayari Group wa kushirikina na Sos Childrens Village Tanzania wamezindua vituo viwili vya shamba la kisasa ambayo yanakwenda kuwa msaada kwa kaya zaidi ya 80 maeneo ya chanika jijini Dar es Salaam katika kujikwamua kiuchumi.
Uzinduzi huo wa vituo hivyo umefanyika jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa kituo cha Taarifa na Maarifa cha Sayari Group Nipaeli Mrutu wakati wakiandaa shamba darasa eneo nguvu mpya katika wilaya ya ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kuzindua vituo hivyo Mkurugenzi Mrutu, amesema kuwa kituo cha Sayari Group kina wanachama 126 ambao wanajishughulisha na Ujasiriamali wa Kilimo cha mboga mboga kwa njia ya kisasa.
"lengo ni kuisaidia Serikali kuinua uchumi katika kujikwamua kiuchumi watanzaia" amesema Mrutu.
Mrutu ameeleza kuwa tofauti na kilimo kituo kinajishughulisha na shughuli mbali mbali ikiwemo ushonaji pamoja na utengezaji wa mageti.
"Kwa sasa kituo kimepata mafanikio makubwa kwa kuongeza matawi mapya mawili ambapo ndani ya vikundi hivyo kuna vijana, wakinamama, wazee pamoja na wajane na wazee" amesema Mrutu.
Amesema kuwa ni vizuri makundi mbalimbali katika jamii wakajiunga na kituo cha Sayari group kwani ni sehemu ya ajira na ujuzi kwa wakazi wa Chanika, Zingiziwa na maeneo ya jirani.
Hata hivyo Mrutu amebainisha kwa kituo chake kinakabiliwa na changamoto mbalimbali, huku akiomba serikali kuwangalia wajane kwa kuwapatia msaada kutokana wameonekana kuwa mazingira sio rafiki katika uchumi.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari gruop Nuru Dilangale, amewataka wananchi wajifunze kilimo cha kisasa (magorofani) kutokana kwa watu wa mjini kimeonekana ndio kilimo rafiki.
Afisa Mradi, Mradi wa kuimarisha Familia kutoka Sos Childrens Villages Tanzania Lukasi Hyera, amesema kuwa wanafanya kazi wapo wanafanya kazi na Sayari Group kwa lengo la kutoa elimu ya Kilimo kwa lengo ya kuzisaidia familia maskini.
Hivyo makala SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA.
yaani makala yote SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/sayari-group-yazindua-vituo-vipya.html
0 Response to "SAYARI GROUP YAZINDUA VITUO VIPYA SHAMBA LA KISASA."
Post a Comment