title : POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA
kiungo : POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA
POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola maesema licha ya kuwa Jeshi la Polisi linapambana usiku na mchana kuwaondoa askari wala rushwa lakini ana taarifa ya baadhi yao wanaendeleza tabia hiyo, hivyo dawa yao ipo jikoni inachemka.
Amesema licha ya kutoa taarifa mara kwa mara kuwataka askari hao kufanya kazi kiuhadilifu kwa kuacha tabia ya kuomba rushwa lakini baadhi ya askari hao hawajamuelewa hivyo atapambana nao mpaka Jeshi hilo litakapokuwa safi.
Lugola amesema anapokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wananchi kuwalalamikia baadhi ya Polisi kufanya matukio hayo ambayo hayakubaliki lakini anawataka askari polisi hao wajue kuwa kati ya maagizo aliyopewa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ni kupambana na rushwa ndani ya Wizara hiyo, hivyo hawezi kumuangusha hata siku moja.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Namibu, Kata ya Neruma, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola alisema baadhi ya polisi wanalichafua Jeshi hilo kutokana na tamaa zao, hivyo ameendelea kusisitiza kuwa, Serikali ya Magufuli ya awamu ya tano siyo ya kuchezewa.
“Jeshi la Polisi linalinda usalama wa raia na mali zao, linapambana na rushwa katika mambo mbalimbali yakiwemo ya ardhi hapa kijijini, hivyo ndugu wananchi mnapopata migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi na mengineyo akikisheni mnatoa taarifa polisi ili muweze kusaidiwa,” alisema Lugola.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akifurahi jambo wakati alipokua anasalimana na Diwani wa Kata ya Nyamihyolo, Mgendi Patrick, wakati Waziri huyo alipopokelewa na mabango na wananchi wa Kijiji cha Mahyolo, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambayo yalikua yana ujumbe mbalimbali. Lugola aliwataka wananchi wa Kijiji hicho wafanye shughuli za maendeleo bila kuvunja sheria za nchi. Pia alitoa onyo kwa baadhi ya askari kuiacha tabia hiyo haraka iwezekanavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Mahyolo, Clifford Bwire, alipokua anajibu maswali kuhusu ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Mahyolo iliyopo Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, kutokuendelea licha ya kua wananchi wa kijiji hicho walichanga fedha. Pia Lugola aliwataka wananchi wa Kijiji hicho wafanye shughuli za maendeleo bila kuvunja sheria za nchi. Pia alitoa onyo kwa baadhi ya askari ambao wanaomba rushwa kwa wananchi kuiacha tabia hiyo haraka iwezekanavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola, akiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano iliyopo Kijiji cha Namibu, Kata ya Neluma, Jimbo la Mwibara, Bunda, Mkoani Mara, wakati Waziri huyo alipofanya ziara shuleni hapo kwa ajili ya kuwasalimia wanafunzi hao pamoja na uongozi wa shule hiyo. Lugola yupo katika ziara ya kuhamasisha maendeleo na pia kuwapa elimu ya ulinzi na usalama jimboni kwake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hivyo makala POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA
yaani makala yote POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/polisi-wachache-wanaolichafua-jeshi-kwa.html
0 Response to "POLISI WACHACHE WANAOLICHAFUA JESHI KWA KULA RUSHWA DAWA YAO IPO JIKONI-LUGOLA"
Post a Comment