NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU

NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU
kiungo : NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU

soma pia


NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU

NA LUSUNGU HELELA
Naibu Waziri Wizara ya  Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu

Naibu Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza  kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa  kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara hiyo  nyeti kwa uchumi wa nchi. Amesema ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi  anazoziongoza ili kujua namna zinavyotenda kazi na  changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumza kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi.   Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii kubadili maslahi ya watumishi hao  na endapo maslahi hayo yatabadilika basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao.

Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na  Utalii ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo. Katika hatua nyingine,  Naibu Waziri Kanyasu ameiagiza Menejimenti ya Mamlaka ya  Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ibuni  vivutio  vipya vya  Utalii vitakavyosaidia  kuongeza  mapato kwa Serikali kwa kuzingatia majukumu makuu ya Taasisi.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akimsikiliza  Mhifadhi ,kuu  wa Mamlaka ya Hifadhi ya enoe la n Ngorongoro, Dkt.Freddy Manongi  wakati  alipowatembelea jana katika  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuzungumza na  kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) akipewa maelezo na Dkt. Maurus Msuha (katikati) wakiwa kwenye sehemu ya kuonea wanyamapori (View point) ya Ngorongoro Kreta wakati alipotembelea jana  kwa ajili ya  kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
 Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  wakati alipowatembelea jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  akipewa maelezo na Juma Hamadi jinsi mfumo wa malipo unavyofanya kazi kwa watalii wanaoingia katika  Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro

                       (PICHA NA LUSUNGU HELELA-WMU) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
  


Hivyo makala NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU

yaani makala yote NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/naibu-waziri-kanyasu-awatoa-hofu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAIBU WAZIRI KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU"

Post a Comment