title : MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI
kiungo : MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI
MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI

MBUNGE wa Korogwe vijijini ndugu Timotheo Mnzava, Novemba 18, 2018 amefanya mkutano wake wa kwanza na wananchi mara baada ya kuapishwa rasmi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma Novemba 6, 2018.
Mkutano huo ambao ulifanyika katika kata ya Makuyuni, Mnzava amewahakikishia wananchi wa jimbo la Korogwe vijijini kutatua kero sugu zilizopo ndani ya jimbo ambapo zile zilizo juu ya uwezo wake kuendelea kuikumbusha serikali kutatua ili wananchi wapate maisha bora.
Aidha Mnzava ameainisha changamoto ya Elimu, Maji, afya na Miundombinu ya barabara ndio vipaumbele ambavyo ataanza kuvishughulikia katika kipindi chake cha kuiongoza Korogwe vijijini.
Mnzava amewahakikishia wananchi kuhusu Korogwe mpya na yenye matokeo chanya inayoenda sambamba na dhamira ya Mh. Rais Dkt John Pombe Magufuli ya kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025.
Mnzava alimalizia kwa kumshukuru rais Magufuli, Wananchi pamoja na chama cha mapinduzi kwa imani waliyonayo juu yake na kumchagua kuwa mbunge atakayeiongoza Korogwe vijijini na kuleta maendeleo yenye tija na endelevu.
Hivyo makala MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI
yaani makala yote MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mrithi-wa-profesa-maji-marefu-aanza.html
0 Response to "MRITHI WA PROFESA MAJI MAREFU AANZA KUUNGURUMA KOROGWE VIJIJINI"
Post a Comment